…………………………………
Serikali kwa kushirikiana na
Kampuni ya Mabey Bridge ya nchini Uingereza wamejipanga kikamilifu
kujenga barabara tatu za juu (Fly Overs) na barabara nne za
watembea kwa lengo la kupunguza msongamano wa foleni jijini Dar es
Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa
mazungumzo hayo na kampuni ya Mabey Bridge ya Uingereza kwa ajili
ya ujenzi wa barabara hizo nchini.
Profesa Mbarawa alisema kuwa
barabara hizo zitajengwa hasa maeneo ambayo yana msongamano mkubwa
wa magari ikiwa ni pamoja na eneo la barabara ya Mwenge.
“Serikali imejipanga kikamilifu
kuhakikisha wananchi wanakuwa na miundombinu iliyobora hasa katika
upande wa barabara za magari na barabara za waenda kwa miguu ili
kuwarahisishia wananchi kuwahi kuwajibika katika maeneo yao ya kazi”.
Mbali na hayo, Waziri Mbarawa
alifanya ziara ya kushtukiza katika Daraja la Nyerere lililopo maeneo
ya Kigamboni kwa lengo la kutaka kujua maendeleo ya daraja hilo na
kumtaka msimamizi wa daraja hilo kuandaa kadi maalumu au
kitambulisho zitakazotumika kwa lengo la kupunguza msongamano wakati
wa kulipia tozo.
vilevile Waziri
aliwataka wananchi kuwa waangalifu na miundombinu ya daraja hilo
na endapo kuna mtu atakaye bainika kuharibu atachukuliwa hatua
kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa faini za gharama ya juu.
“kuanzia sasa kunatakiwa kuwepo
na faini kali kwa mtu yeyote atakaye haribu miundombinu ya daraja
hili kwa lengo la kulifanya daraja lidumi kwa muda mrefu” alisisitiza
Waziri Mbarawa
Kwa upande wake Msimamizi
Mkuu wa daraja la Nyerere, Gerald Sondo alisema wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya madereva wa daladala kushindwa kutumia
daraja hilo na kudai kuwa tozo ni kubwa.
Vilevile Waziri huyo alifanya
ziara katika eneo la ujenzi wa mtambo wa Mafuta kutoka kwenye meli
kabla ya kuingia kwenye matanki (Flow Meter) kuona maendeleo ya
ukarabati wa mtambo hio uliyoharibika hivi karibuni kutokana na mvua
kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kumtaka mkandarasi
kuhakikisha eneo hilo linazungishiwa ukuta ili kuziba mitambo
hiyo.
Tags
HABARI KITAIFA