Ushauri huo umetolewa na
mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,ambapo amesema kwakuwa Yanga ni klabu
kubwa yenye wanachama na mashabiki wengi nchini, wapiga kura hawana budi
kuzingatia kuwa hali ya utulivu inatawala katika zoezi hilo kuhimu kwa
mustakabali wa klabu yao.
Amewashauri pia wapiga kura
kufanya uamuzi sahihi wa kuchagua viongozi wanaowaona wanafaa ili
kuendeleza hali ya utulivu iliyopo kwenye klabu hiyo ambayo ndiyo
mabingwa wa ligi kuu na kombe la shirikisho.
Amesema kama wanachama
watashawishika na kujikuta wanashindwa kudhibiti hisia zao kwa kuleta
vurugu,basi hali hiyo inaweza kuwaingia katika mfarakano mkubwa unaoweza
kuharibu hata mipango yao katika michuano ya kimataifa ambapo Yanga
imefanikiwa kutinga katika hatua ya makundi.
Kasongo amewahakikishia wana
Yanga kuwa chama chake kipo tayari kufanya kazi kwa karibu na viongozi
watakaochaguliwa ili kuendelea kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuwa mfano
wa kuigwa katika maendeleo ya soka.
Yanga itafanya uchaguzi wake
kesho juni 11,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar es
salaam kuanzia majira ya asubuhi.
Tags
MICHEZO KITAIFA