……………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe.Paul Makonda atazindua maonyesho ya kwanza ya simu original katika
viwanja vya Posta jumamosi ya Tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa 3 asubuhi
mpaka saa 12 jioni.
Lengo kuu la kufanyika kwa
maonyesho hayo ni kuwapa elimu wateja wa simu kujua ipi ni simu fake na
ipi ni original kutoka kwa makampuni hayo ya simu,pia kwa kushirikiana
na TCRA watatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya simu na mitandao ya
kijamii.
Lengo la tatu ni kuhakikisha wateja wanajipatia simu original kwa bei nafuu kabla ya simu fake kuzimwa tarehe 16 mwezi huu.
Nae Kaimu Katibu mtendaji wa
Baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano(TCRA-CCC),Mary Msuya
amewashauri watumiaji wa simu nchini kununua simu katika maduka ya simu
na kuomba risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua
miezi 12.
Aidha aliwataka wafanyabishara
wasio waaminifu kuacha mara moja kuingiza bidhaa feki nchini kwa njia za
panya kwani serikali iko makini katika kusimamia suala hilo.
Kwa upande wake mwakilishi wa
makampuni ya simu Meneja mauzo wa kampuni ya Tecno Bw.Fred Kadilana
ametoa wito kwa watumiaji wa simu kuja kwa wingi ili kujipatia simu
zenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni mbalimbali.
Wateja wa simu za mkononi
watajipatia simu original kutoka katika maonyesho hayo kwa bei nafuu
kutoka kwa makampuni ya simu ya Samsung,Tecno,Startimes,Huawei na Itel
uku kukiwa na ushiriki wa makampuni ya simu ya Vodacom,Tigo na TTCL.
Katika maonyesho hayo Taasisi
mbalimbali za serikali zitashiriki kama mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA), Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano
(TCRA-CCC) na Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Tags
HABARI KITAIFA