Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira Mhe. Jenista
Mhagama akitoa maelezo Bungeni leo kuhusu hatua zitakazochukuliwa na
Serikali dhidi ya waajiri wote wanaoshindwa kuwasilisha michango ya
waajiriwa wao katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuwa watachukuliwa hatua
kali za kisheria ambapo tayari Serikali iko kwenye hatua za mwisho
kukamilisha mchakato wa kuunda kikosi kazi kitakachoshughulikia swala
hilo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mh. George Masaju leo Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira, Mhe. Jenista
Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde leo
Bungeni Mjini Dodoma.