BANDA MEDIA BLOG

MGONJWA WA AKILI AUA MWENZEKE KATIKA HOSPITAL YA MIREMBE DODOMA




Mmoja wa wagonjwa wa Akili
Wauguzi katika hospital ya Mirembe
Sehemu ya mji wa Dodoma
Dodoma ipo katikati ya Nchi
IMEANDALIWA NA BANDA BLOG

MGONJWA wa akili anayetibiwa katika hospitali ya Milembe iliyopo mjini Dodoma  Stella Mbalwa  amemuua mgonjwa mwenzake Halima chedi kwa kumpiga na kuni kichwani.
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ASP Lazaro Mambosasa alisema tukio hilo lilitokea june 19 majira ya saa 3.30 asubuhi.

Kamanda alisema tukio hilo lilitokea wakati wagonjwa hao wakinywa uji hospitalini hapo ambapo Stella alichukua moja ya kuni zilizokuwa jirani na eneo hilo na kumpiga nayo marehemu kichwani ambapo marehemu alipoteza maisha hapo hapo.

Wakati huo huo Kamanda Mambosasa alisema Mwili wa mzee mmoja wa makamo anayekisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 70 na 77 ambaye hakutambuliwa jina wala makazi yake uliokotwa jirani na kanisa la roma kata ya hazina manispaa ya Dodoma majira ya saa 2 asubuhi   

 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG