Mhe. Amani K. Mwenegoha ameyasema hayo jana akikanusha taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwanahalisi na mwandishi Ansbert Ngurumo
toleo na: 341 la Mei 30 mwaka 2016 siku ya Jumatatu ukurasa wa 10 na
11. Alisema katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari kinachosema “Ngono na Mwanafunzi yaleta msukosuko Ushirombo”
mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Bukombe nimetuhumiwa kutumia madaraka yangu
vibaya kwa kumlinda na kumkingia kifua Afisa Tarafa wa Siloka Bw. Tumbo
John Madaraka.
“Sikuwahi Kupokea barua
yeyote kutoka kwa Matayo Paschal wala kuamrisha akamatwe ,pia sikuwahi
kuzungumza na mwandishi yeyote kuhusu mtoto huyo,wala sijapokea
taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi Bukombe kuhusu mtoto huyo wala
malalamiko yoyote kutoka kwa wazazi,mlezi au Mwalimu Mkuu wa Shule
aliyosoma mwanafunzi huyo” alisema Mkuu wa Wilaya Mhe. Amani Mwenegoha akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana.
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Wilaya ya Bukombe amekemea na kulaani kitendo cha mwandishi wa gazeti
la Mwanahalisi kuandika habari bila kuzingatia maadili ya kiuandishi
kwa kufika eneo la tukio na kuonana na walengwa sio kuandika habari za
kupelekewa au kusikia mtaani, angezingatia kupata taarifa kwa pande
zote mbili ili kupata taarifa zenye ukweli,uwazi na uhakika”.
Pia ametoa wito kwa waandishi wa
habari nchini kuwa wazalendo na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa nchi
yetu kwa kufichua uovu utakaorudisha nyuma maendeleo ya jamii yetu
badala ya kuweka vibonzo visivyowakilisha maslahi ya nchi yetu na
kuvunja moyo juhudi zinazofanywa na Rais wetu za kuinua Uchumi.
Wakati huo huo, Mkuu wa
wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha amesisitiza wazazi, walezi na
jamii kwa ujumla kutoa taarifa kwa vyombo vya serikali haraka kadri
inavyowezekana inapotokea wana tatizo linalohusiana na watoto wao
wanapokutana na changamoto ambazo serikali inaweza kushughulikia na
imekua ikifanyika hivyo pale ambapo mzazi,mlezi au jamii inapotoa
malalamiko au taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ambapo yamekua yakishughulikiwa
na sheria imekua ikichukua mkondo wake.
Tags
HABARI KITAIFA