BANDA MEDIA BLOG

MSIBA MKUBWA WA DUNIA!!!! MOHAMMAD ALI BONDIA WA ZAMANI AFARIKI DUNIA


Bondia wa zamani Muhammad Ali, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 74. Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa familia yake, Ali amekufa baada ya kuugua ugonjwa wa Parkinson kwa miaka 32. 

Bob Gunnell, msemaji wa familia ya Ali amesema gwiji huyo wa zamani wa masumbwi duniani alikuwa amelazwa katika hospitali ya Phoenix katika jimbo la Arizona, akiwa na matatizo ya kupumua wiki hii. 

Aliwahi kulazwa hospitali mwaka 2014 baada ya kuugua homa ya mapafu, na kisha akalazwa tena mwaka uliopita kutokana na maambukizi katika njia ya kupitishia mkojo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG