LEO timu yetu
ya Taifa, Taifa Stars iliyopo kundi G katika michuano ya kufuzu kwa
fainali za Kombe la Mataifa Afrika inaumana na Misri katika mchezo
utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kundi hilo
linaundwa na timu nne huku kukiwa na jumla ya makundi 13 ya timu nne nne
ambayo kupitia makundi hayo ndipo yatatoka majina halisi ya timu,
ambazo zitacheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwakani nchini
Gabon.
Timu hizo
zimekuwa zikicheza michezo ya ndani na nje ya nchi kuanzia Juni 2015
hadi Septemba mwaka huu na kundi hilo lina timu nne, ambazo ni Nigeria,
Misri,Tanzania pamoja na Chad, ambayo ilijitoa.
Kujitoa kwa
Chad Lakini hata hivyo inaonekana kuwa Machi 27 mwaka huu, Chad
ilitangaza kujitoa katika michuano hiyo kutokana na uhaba wa fedha
unaoikabili nchi hiyo.
Kutokana na
taratibu ni kwamba kwa timu ambayo inajitoa basi ndio hata zile pointi
ilizokuwa amezipata zinapokwa. Lakini pia hata ile michezo ambayo timu
hiyo ilikuwa imepangwa kucheza nazo inafutwa.
Mchezo huu wa
Misri na Taifa Stars unachezwa huku timu ya Nigeria, Super Eagles ikiwa
tayari imeshafahamika kuwa imeshindwa kufuzu katika michuano hiyo
itakayochezwa Gabon.
Hiyo ni baada
ya kufungwa 3-0 na Misri katika mchezo wao huo uliochezwa katika Uwanja
wa Borg El Arab uliopo, Alexandria. Pia katika mchezo wa pili, Misri
ilitoka sare ya 1-1 katika mchezo uliokuja kuchezwa Kaduna, Nigeria.
Wamisri hao wanakuja kucheza mchezo wao huo wa leo wakiwa na ghadhabu ya ushindi kutokana na kukosa mara tatu ubingwa huo.
Kwa sasa wakiwa
wanaongoza kundi lao wakiwa na pointi saba wanaonekana ni dhahiri kuwa
wamejipanga vema kwa mchezo wao huo wa leo hasa kutokana na ushindi
ilioupata katika michezo iliyopita.
Kufuzu kwa Misri Misri inahitaji sare tu dhidi ya Taifa Stars ili iweze kukata tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Gabon 2017.
Stars inatakiwa
kucheza ikiwa na tahadhari kubwa ya wachezaji wa Misri, ambao wengi wao
wanatoka katika klabu kubwa nchini humo kama Al-Alhy, Zamalek na
zingine. Pamoja na Misri kuonekana kufanya vizuri, lakini Taifa Stars
inaweza kuifunga Misri endapo tu itagangamala na kucheza kwa ari kubwa.
Endapo Stars
itashinda leo, basi itarejesha matumaini ya kufuzu kwa mara ya pili
fainali hizo baada ya zile za mwaka 1980 nchini Nigeria ilizocheza kwa
mara ya mwisho.
Stars katika
mchezo wake wa kwanza ilifungwa na Misri 3-0 mwaka jana wakati ikiwa na
kocha wake Mart Nooij na ndicho kilikuwa chanzo za kocha huyo kuondolewa
kukinoa kikosi hicho. Huku kwa sasa kikiwa chini ya Charles Mkwasa
ambaye ni mzawa na alipewa jukumu la kuinoa timu hiyo kwa sasa anasema
kuwa ana imani kuwa anaweza kuwanoa mafarao hao wa Misri.
Ni dhahiri kuwa
wachezaji wa Stars wanaweza kucheza wakiwa na nia ya dhati hasa zaidi
kwa kuwa wanakuwa wakichezea uwanja wa nyumbani hivyo wana kila sababu
ya kushinda. Mkwasa anasema kuwa ushindi ni lazima kwa kuwa wachezaji
wake wamekuwa wakitumia muda mwingi zaidi kujituma kimazoezi. Alisema
kuwa mchezo huo kazi moja kubwa itakuwa ni ushambuliaji na pia uchezaji
unaozingatia nia na kujituma. Anasema kuwa kwa sasa wachezaji wote wapo
salama na wanaendelea na uchezaji wa hali na mali wakiwa mazoezini.
Aliongeza kuwa
watahakikisha kuwa wanashambulia zaidi ili kufanikisha adhma yao ya
ushindi. “Tunatambua nafsi ya mchezo huu kwa timu yetu na taifa zima kwa
ujumla na wachezaji hawa wapo katika hali nzuri ya kimchezo na hakuna
majeruhi hadi sasa,” alisema kocha huyo. Mchezaji wa timu hiyo
anayechezea timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anasema kuwa mchezo
wa kesho ni ushindi tu.
Anasema kuwa
wachezaji wamejipanga vya kutosha na kuwa ushindi ni lazima kwa kuwa
hakuna sababu ya kufungwa katika mchezo huo. “Wachezaji wapo poa kabisa
kocha naye yupo safi na wachezaji wanahitaji ushindi kitu ambacho leo ni
lazima waone tukifanya hivyo,” alisema. Ni vema kwa wananchi kujitokeza
kwa wingi kuunga mkono timu yetu kwa kuwa wanaweza kufanya vema iwapo
tukiwahamasisha.
Katika hili ni
vema kwa wote kwa pamoja tukaungana kuanzia na mwenye ngoma, kanga,
tarumbeta na mengineo yote kujitokeza kwenda kahamasisha
Tags
MICHEZO KITAIFA
