Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa na viongozi wa Taifa la Nigeria na Shirika la Makazi la
Afrika Jijini Abuja wakati ukipigwa wimbo wa Taifa la Nigeria katika
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika.
………………………………………………………………………………………………………………………
Katika kutambua mchango wa
Tanzania katika uendelezaji wa makazi ya watu na kuweka mbele utu wa
binadamu wa mahitaji ya msingi ikiwemo nyumba, wajumbe kutoka nchi 44 za
kiafrika waliohudhuria Mkutano wa 35 wa Shirika la Makazi la Afrika
Jijini Abuja Nigeria, kwa pamoja wameiteua na kuiidhinisha Tanzania kuwa
mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Shirika hilo utakaofanyika mwaka 2018.
Katika Mkutano Mkuu wa Abuja
changamoto iliyojitokeza ni uwezo wa nchi za kiafrika wa kuwapatia
wananchi wake nyumba za gharama nafuu, huku wajumbe wakitoa rai kwa
serikali zao kuainisha vigezo vya kutambua nyumba ya gharama nafuu.
Aidha, wajumbe wa Mkutano huo wanaona changamoto kubwa ya wananchi wengi
wa Afrika kuweza kumiliki nyumba ya gharama nafuu ni uwezo mdogo
unaotokana na vipato vidogo, kutokuwepo sera ya kuwezesha raia kumiliki
nyumba za gharama nafuu, kukosekana kwa miundombinu katika makazi ya
gharama nafuu, riba kubwa za mikopo ya ujenzi wa nyumba nafuu na
ukosefu wa ardhi ya kujenga nyumba hizo.
Kwa ujumla changamoto za nchi za
kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana
na kilio kikubwa katika nchi hizo ni kuwepo makazi holela hata baada ya
nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. Hivyo, Mkutano Mkuu huu
umeazimia nchi wanachama kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya
nyumba kwa kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na
maisha bora ya watu.(Habari za mkutano huo katika picha na Muungano
Saguya, Abuja, Nigeria)
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula (wan ne kulia) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa
katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique).
Wengine ni Waziri wa Nishati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde
Fashiola (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shelter Afrique Bw. James
Mugerwa (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shelter
Afrique Bw. Jean-Paul Missi (wa kwanza kulia).
Mkurugenzi
Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili
kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter
Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali
zilizowasilishwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa meza kuu baada ya Tanzania kuteuliwa na kuidhinishwa na
Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique Jijini Abuja kuwa mwenyeji wa
Mkutano wa 37 utakaofanyika nchini Tanzania mwaka 2018.Kulia kwa Naibu
Waziri ni Waziri wa NIshati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde
Raji Fashola ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Wajumbe
kutoka nchi 44 za Afrika na wageni waalikwa kutoka nchi na mashirika
mbalimbali ya Kimataifa wakiendelea na Mkutano wa 35 wa Shirika la
Makazi la Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton Jijini
Abuja, Nigeria. Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni
katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya
kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la
Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline
Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni
katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya
kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la
Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kutokana na hali ya amani katika nchi
hiyo, Naibu Waziri alipata ulinzi wa kutosha kama inavyoonekana
alipopiga picha ya pamoja na walinzi walioandamana na wageni kutoka nchi
mbalimbali katika ziara hiyo. Tudumishe amani yetu Tanzania
Mchoro
huu juu na chini unaonyesha taswira ya mji wa kisasa unaotabiriwa kuwa
Dubai ya Nigeria unaojengwa nje kidogo ya Jiji la Abuja ujulikanao kama
Centenary City Abuja ambao wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika
waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika waliweza
kuutembelea na kujionea ndoto ambayo wanigeria wameamua kuitekeleza.
Wajumbe
wa Mkutano wa 35 wa Shelter Afrique wakiwa katika eneo la centenary
city unaotarajiwa kuwa mji wa kibiashara Jijini Abuja mji ambao
unajengwa na serikali ya Nigeria kwa kushirikiana na sekta binafsi.