YAHYA NJENGE
Baada ya kuona michezo ya
ufunguzi ya Ligi Kuu ya Tanzania bara, kisima cha hisia zangu kimeguswa
sana na matokeo yaliyo jitokeza pale Manungu Tuliani, kikosi cha Mtibwa
Sugar kikichapwa bao moja kwa bila na Ruvu Shooting, Kwahakika rekodi za
Mtibwa kwa miaka ya karibuni imekuwa ikifanya vizuri katika michezo ya
awali lakini msimu huu hali ni tofauti.
TATIZO NI NINI?
Changamoto kubwa kwa Mtibwa Sugar ni kutolitumia vyema dirisha la
usajili lililopita, Mtibwa wamejitengenezea utamaduni wa kuuza sana
wachezaji wanao watengeneza na kila msimu wamekuwa wakibaki kwenye ubora
wao, Hali ni tofauti kidogo msimu huu mtibwa imewapoteza wachezaji
muhimu kama beki Andrew Vicent aliyeenda Yanga, Shiza Kichuya na
Muzamiru Yasini waliojiunga na timu ya Simba.
Kwa hakika kupoteza mchango
wa nyota hawa ni pigo la moyo kwa mtibwa, Nje ya nyota hao kocha
waliyedumu naye kwa zaidi ya miaka mitatu Mecky Mexime nae ametimkia
Kagera Sugar, Kwahakika kuondoka kwa kocha aliyeifahamu vizuri Mtibwa
kutaitesa timu hii.
HATIMA YAKE
Ni mapema sana kusema chochote kwa sababu ni mchezo mmoja tumeona
wamecheza chini ya kocha Salumu Mayanga, lakini wasipoangalia huu
unaweza kuwa msimu mgumu zaidi kwao. Na kama walivyoshuka daraja vigogo
Costal Union haitoshangaza na wao likiwakuta hilo.
Tags
MICHEZO KITAIFA