MOSHI SHABANI MALLEMA
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais
John Pombe Magufuli imejitahidi kwa hali na mali kupitia wadau
mbalimbali wa masuala ya Maendeleo, kufanikisha kuwa suala la uhaba wa
madawati linakuwa historia kwa shule zote hapa nchini, ambapo kwa Mkoa
wa Dar es Salaam zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi cha kuwa na madawati
mengine ya ziada, ambapo wilaya ya Ilala ina madawati ya ziada zaidi ya
3000, lakini kumekuwa na matumizi ambayo si sahihi kwa madawati hayo.
Akizungumza na Tovuti hii Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameeleza kuwa madawati yanayosambazwa na
Serikali, kwenye shule mbalimbali hapa nchini ni kwa ajili ya wanafunzi
pekee, hivyo yasitumike kwa matumizi mengine kama kukodisha kwa ajili ya
shughuli za kisiasa, kidini na kijamii.
Huku akisisitiza kuwa Serikali inatumia
gharama kubwa kwa ajili ya suala la madawati, hivyo kuyatumia madawati
hayo kinyume na utaratibu ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali katika
kuwapatia elimu bora yenye mazingira rafiki watoto wa Tanzania, kwani
madawati mengi yameripotiwa kuharibika kutokana na matumizi ya namna
hiyo.
Ambapo amesema kuwa anapiga marufuku matumizi yasiyo rasmi kwenye madawati, ambayo yametengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi ambao walikuwa wanateseka kwa kukaa chini, na kuahidi kuwachukulia hatua wote watakao kwenda kinyume na agizo hilo.
Tags
ELIMU