BANDA MEDIA BLOG

USHINDI SERENGETI BOYS, SALAMU TOSHA KWA TIMU YA TAIFA YA CONGO

serengeti-boys-wakishangilia-2016_l6bf90p7ic0b14w59v716vnko  BURHANI MOHAMED

Wakicheza pungufu kwa muda mwingi wa mchezo kufuatia kadi nyekundu aliyoipata kiungo wao Ally Hamisi Ng’anzi, dakika ya 44 vijana wa Serengeti Boys waliigagadua Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Afrika kusini maarufu kama Amajimboz mabao 2-0 yakifungwa na Mohamed Rashid Abdallah kipindi cha kwanza na Muhsin Malima Makame kipindi cha pili.serengeti-boys-2016_xdanl02rzd9h1iao9ghn6qgvm

Kwa ushindi huo sasa Serengeti Boys wanasonga mbele hatua inayofuata kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya sare ya 1-1 waliyoipata Afrika Kusini katika mchezo wa awali uliofanyika wiki iliyopita.BAKARI SHIME

Kwa ushindi huo ni kama Mwalimu Bakari Shime ametuma salamu kwa timu ya Taifa ya Vijana ya Congo ambayo yenyewe imeichapa Namibia 3-0 nakutinga hatua ya mwisho ya mchujo, ambapo watavaana na Serengeti Boys.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG