BURHANI MOHAMED
Katika kile kinachoonekana ni kuguswa
na suala la Sudan ya Kusini, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John
Kerry amefika jijini Nairobi nchini Kenya kwa ziara yenye lengo la
kudumisha amani nchini Sudan kusini.
Kerry atakutana na Raisi wa Kenya Uhuru
Kenyatta na kufanya nae mazungumzo kisha atazungumza na Mawaziri wote
wa mambo ya nje wa Afrika Mashariki lengo kuu ni kuhakikisha amani
inadumishwa katika taifa hilo changa zaidi Duniani.
Kerry
ameonekana kuwahurumia watu wa Sudan ya Kusini kwa mateso wanayoyapata
kutokana na mgogoro wa nchi hiyo ambao bado ufumbuzi wake umekuwa
kitendawili.
Tags
KIMATAIFA