Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa, Zelothe Stephen pamoja na Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. John
Gurisha kusimamia na kulinda fedha za CHF zinazochangwa na wananchi na
kuhakikisha zinatumika kama zilivyokusudiwa.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye jimbo la Kwela, Tarafa ya Mtowisa
wilayani Sumbawanga.
“Kitendo cha kula fedha
zinazochangwa na wananchi kwa lengo la kupata huduma za afya kinawafanya
wakatetamaa ya kuendelea kuchangia mfuko huo. Kama wako watumishi wenye
tabia hizo waache mara moja,” amesisitiza.
Mbali na kutoa agizo hilo kwa
uongozi wa mkoa wa Rukwa, pia Waziri Mkuu amewataka wananchi kujiunga na
CHF kwa sababu mfuko huo utawawezesha kupata huduma za matibabu bure
wao na familia zao katika kipindi cha mwaka mzima.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema
barabara ya kutoka Ntendo hadi Muze ye urefu wa kilometa 85 itajengwa
kwa kiwango cha lami ili iweze kupitika kwa urahisi na kuwawezesha
wananchi kupata huduma kwa wakati.
“Mimi nilidhani mlima wa Kitonga
ndio mkali kuliko yote na eneo la Sekenke ndio linatisha zaidi!. Kumbe
barabara ya kuja huku Mtowisa ndiyo inatisha zaidi kuliko zote. Lazima
tuweke lami ili iendelee kupitika kwa urahisi zaidi,” amesema.
Akizungumzia ombi lililotolewa na
mbunge wa jimbo la Kwela, Ignas Malocha la kutaka tarafa hiyo ya Mtowisa
kuwa wilaya au halmashauri, Waziri Mkuu amesema analichukua na kwenda
kulifanyia tathmini na majibu atayapata kupitia uongozi wa mkoa.
Malocha alisema jimbo la Kwela
linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya miundombinu ya barabara
hali inayosababisha wananchi kushindwa kusafirisha mazao yao kwa
urahisi.
Pia aliomba ukanda huo wa bonde la
mto Rukwa upandishwe hadhi na kuwa wilaya au halmashauri ili kusogeza
huduma za kijamii karibu na wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala
wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Rukwa, Mhandisi Masuka Mkina
ameelezea mkakati wa kuboresha miundombinu ya barabara mkoani hapa
ikiwemo ya kutoka Ntendo hadi Muze wilayani iliyopo wilayani Sumbawanga.
Mhandisi Mkina amesema Serikali
imetenga jumla ya sh. milioni 170 kwa ajili ya kuweka zege kwa ajili ya
kurahisisha upandaji wa mlima hasa kwenye eneo la Kizungu katika
barabara ya kutoka Ntendo hadi Muze.
Tags
AFYA