Mkuu wa Idara ya Mionzi katika
Hospitali ya Taifa wakati Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akieleza
jambo kwa waandishi wa habari leo.
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika
hospitali hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya mashine
ya MRI kuanza kufanya kazi. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa MRI (MRI
Technologist), Joshua Job na Daktari Bingwa wa Mionzi, Mussa Ndukeki wa
hospitali hiyo.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano uliofanyika leo kwenye hospitali hiyo.
Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Medadi Mallaya akimuhudumia mgonjwa leo.
……………………………………………………………………..
Na John Stephen, MNH
Dar es Salaam, Tanzania. Mashine
ya MRI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepona baada ya
kuharibiika tarehe 24/08/2016. Mashine hiyo iliharibiika baada ya
kutokea hitilafu ya umeme. Tangu mashine hiyo imepona tayari wagonjwa 52
wamepatiwa kipimo cha MRI.
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk
Flora Lwakatare amesema baada ya mashine hiyo kuharibiika, mafundi wa
Philips kwa kushirikiana na mafundi wa Muhimbili walibadilisha betri
zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hiyo.
“Tarehe 26/08/2016, mafundi
walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika
mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu.
Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module
kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips
wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi,” amesema Dk Lwakatare.
Mmoja wa ndugu wa wagonjwa,
Lazaro James, mkazi wa Singida amesema kwamba tangu kuharibiika kwa
mashine ya MRI alikuwa akiisubiri na kwamba amefurahi baada ya kurejea
kwa huduma hiyo.
“Tunashukuru huduma za MRI
zimerejea hapa Muhimbili, gharama zake ni nafuu kuliko kuliko kupata
matibabu nje. Jambo lingine napenda kuwapongeza madaktari na wauguzi kwa
utendaji bora.
Naye Hawa Hussein mkazi wa
jijini Dar es Salaam, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwa
imekuwa ikitoa huduma bora kwa wagonjwa.
Hawa ameuopongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya juhudi za kuiwezesha mashine hiyo kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa.
Amesema kwamba madaktari wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hivyo wana imani wataendelea kupata huduma bora na kwa wakati.
Tags
AFYA