Rais
Uhuru Kenyatta leo amepuuzia ripoti za vyombo vya habari vya Kenya
zinazoashiria kuwepo kwa mgogoro baina ya Kenya na Tanzania.
Akiongea
wakati akizindua temino ya pili katika bandari ya Mombasa, rais
Kenyatta amekanusha kuwepo kwa aina yoyote ya mgogoro, na kusema nchi
hizo zinategemeana.
“Nimesoma
magazeti na kuangalia televisheni zikiashiria kuwepo mgogoro baina
yetu, lakini nataka kuwaeleza wazi kuwa Kenya na Tanzania hazipo kwenye
mgogoro wa aina yoyote,” alisema Kenyatta.
Rais Kenyatta amesema uchumi wa mataifa haya mawili unaingiliana na ni kwa manufaa ya wananchi wa Kenya na Tanzania.
Tags
KIMATAIFA
