Wachezaji wa timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya wakiwa katika mazoezi.
Alichokisema Kocha Phiri baada ya mchezo dhidi ya Mbao Fc hiki hapa
…………………………………………………..
BAADA ya safari ndefu ya saa
kadhaa, kikosi cha Mbeya City Fc tayari kimewasili jijini Mbeya
kujiwinda na mchezo ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam
Fc uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine.
Muda mfupi uliopita meneja wa
kikosi hiki Geoffrey Katepa ameimbia mbeyacityfc.com kuwa Mwalimu Kinnah
Phiri ameamua kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake ili waweze
kupumzika kutokana na uchovu wa safari ndefu na siku ya kesho jioni
wataingia kwenye uwanja wa Sokoine kuanza mazoezi ya matayarisho ya
mchezo huo wa jumamosi.
“Mwalimu ametoa mapumziko siku
ya leo hii ni kwa sababu tumekuwa na safari ndefu kutoka Mwanza
tukipitia Tabora, hivyo mazoezi ya matayarisho ya mchezo ujao yataanza
kesho jioni, jambo muhimu ni kwamba tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha
kupata matokeo mazuri kwenye michezo yetu mitatu ya mwanzo wa msimu,hili
limetufanya kuongoza ligi kwa mara ya kwanza, jambo ambalo pia
limetuongezea morali kubwa ya kushinda dhidi ya Azam Fc jumamosi”
alisema.
Akiendelea zaidi Meneja Katepa
alisema kuwa kitengo cha utabibu cha City kinachoongozwa na Dr Joshua
Kaseko kimesibitisha kuwa wachezaji wote wako kwenye hali nzuri kwa
maana ya hakuna aliye majeruhi na baada ya mapumziko ya leo wote
watakuwa tayari kwa mazoezi ya kujiandaa kucheza mchezo wa jumamosi.
“Jopo la madaktari wetu
wamenithibitishia kuwa kikosini hakuna mchezaji mwenye majeraha, wote
wana hali nzuri hivyo baada ya kupisha mapumziko ya leo wote watakuwa
tayari kwa mazoezi ya matayarisho ya mchezo”. alimaliza.
Kwenye michezo mitatu iliyopita
City ilifanikuwa kuibuka na pointi 7, kufuatia suluhu ya bila
kufungana na Kagera Sugar na baadae kuiadhibu Toto Africans bao 1-0 na
mwisho kuhitimisha kwa kuifunga Mbao Fc bao 4-1 na kushika usukuni wa
ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Tags
MICHEZO KITAIFA