Na.Alex Mathias.
Timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera imetamba kupeleka kilio kwa matajiri wa jiji la Dar es salaam Azam FC mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotarajiwa kuchezwa siku ya Kesho kwenye uwanja wa Kaitaba.
Akizungumza na FULLSHWANGWEBLOG,Kocha Mkuu wa Kagera Sugar,Mecky Mexime,amesema kuwa wamejiandaa na kushinda mchezo huu ili kurejesha imani kwa mashabiki pamoja na morali kwa wachezaji kutokana na kupokea kichapo cha aibu cha mabao 6-2 toka kwa Mabingwa watetezi Yanga.
“Wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi tumejipanga kupata ushindi na pia tunajua Azam FC ni timu bora kwa sasa ili sisi wametukuta tuna maumivu makubwa hivyo lazima waache alama zote tatu muhimu haijalishi tutapata mabao mangapi ila tutashinda na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufukuzia ubingwa”alisema Mexime
Kagera anakutana na Azam Fc akiwa ametoka kupokea kichapo cha mabao 6-2 wakati matajiri wametoka kupata ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya vibonde wa Ligi JKT Ruvu ambao wanaonekana kusuasua.Timu hizi zinakutana huku zikiwa zimecheza mechi 12 na Kagera Sugar wapo katika nafasi ya nne ya msimamo kwa kuwa na alama 18 wakati matajiri Azam Fc wakiwa na alama 16 na kushika nafasi ya sita na Simba bado anaongoza Ligi ya Tanzania bara kwa alama 29.
Tags
MICHEZO KITAIFA
