BANDA MEDIA BLOG

STAND UNITED YATUMA SALAMU KWA SIMBA HUKU IKITAMBA NA REKODI YA KUWANG’OA VIGOGO CCM KAMBARAGE.

indexNa.Alex Mathias,Dar es salaam.
Kikosi cha wapiga debe Stand United kimeanza kuitangazia vita timu ya Simba ambayo tayari imeshatua mkoani Shinyanga kucheza na wenyeji wao Mwadui FC Jumamosi hii pamoja na wapiga debe.
Kocha wa Stand United, Athumani Bilal amesema wanajua ugumu wa mechi dhidi ya Simba, lakini wanachotaka ni alama tatu.
Simba itacheza na Stand United Novemba 6 ikiwa ni siku chache baada ya kucheza na Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Stand United ndiye timu pekee ambayo imeshinda dhidi ya vigogo ambao ni Yanga na Azam FC na wote imewafunga kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kwa kila timu kupokea kichapo cha bao 1-0.
“Lazima iwe mechi ngumu, hata sisi tunalijua hilo. Lakini kikubwa kwetu tukiwa hapa nyumbani tunachotaka ni pointi tatu,” alisema Bilali.
Stand ambayo imecheza mechi 12 na kujikusanyia alama 21 nafasi ya tatu na ikiwa imepoteza mchezo mmoja na imekuwa ngumu kufungika ikiwa katika uwanja wao wa nyumbani kutokana na kuwapa vipigo unapotua hapa hivyo wana imani kuwa ni zamu ya Mnyama kuacha alama tatu na kuvunja rekodi yao ya kutopoteza hata mchezo mmoja wakiwa chini ya Joseph Omog.
Hata hivyo Kocha wa timu ya Simba Joseph Omog akzungumza akiwa huko Shinanga alinukuliwa na mtandao huuo akisema.
“Nia yetu ni kuendelea kupata matokeo mazuri kwa kila mechi tunayokutana nayo na sio kwamba tunadharau wapinzani ila msimu huu tumejiandaa kutwaa ubingwa mapema na hiyo ndio kiu ya wanasimba”.
“Tumekuja kupambana na kuondoka na alama zote kwa sababu tuna mechi mbili dhidi ya  Stand United na Mwadui FC hivyo hatukuja  kutalii na tunajua michezo yote itakuwa migumu kwetu ila wachezaji wangu wapo kwa ajili ya kupata ushindi”alisema Omog

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG