Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la
JKT Mgulani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti
katika jiji la Dar es Salaam
zilifanyika.
zilifanyika.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January
Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti
iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la
Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti
jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan.
Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya
kilwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar
es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga
na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure
kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure
kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………….
Benjamin Sawe-Maelezo-Dar es Salaam
mefahamika kuwa hewa ya ukaa ina
asilimia kubwa katika gesijoto hivyo kusababisha kumong’onyoka kwa ozoni
na kupelekea kuongezeka kwa kiasi cha nyuzi joto duniani na udororaji
wa uchumi wa nchi
Hayo yamebainishwa na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan katika
uzinduzi wa kampani ya upandaji miti ijulikanayo kama Mti Wangu katika
mkao wa Dar e Salaam.
Mhe. Suluhu alisema kwa kutambua
athari za ongezeko la gesi joto hususani hewa ya ukaa serikali kupitia
mkoa wa Dar es Salaam imekuja na kampeni ya kupanda miti ili kukabiliana
na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam
unazalisha tani 4500 kwa kila siku zitokanazo na gesi za viwandani,
vyombo vya usafiri, taka ngumu za viwandani na majumbani ikiwa ni pamoja
na uchomaji na utupaji taka hovyo hivyo kupelekea serikali kwa
kushirikiana na wadau kuanzisha kampeni hiyo jijini Daar es Salaam.
Alizitaja sababu nyingine za
kampeni hiyo kuanzia Dar esSalaam ni pamoja na makadirio ya ongezeko la
wakazi kufikia 5,895,791 kwa mwaka 2017 hivyo kusababisha kuongezeka
kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa hewa ya ukaa kutokana na kuongezeka
kwa mahitaji mbalimbali ya shughuli za binadamu na viwanda kwa ujumla.
Alisema tafiti mbalimbali
zimeonyesha hewa ya ukaa inaongezeka jijini Dar es Salaam kutokana na
ongezeko la viwanda na idadi kubwa ya wakazi ambapo kwa mwaka 2015
utafiti umeonyesha mkoa huo una viwanda 1854 kati ya hivyo 480 ni
vikubwa na 1374 ni vidogo.
“Nawaagiza viongozi wa Serikali,
taasisi binafsi, Asasi za kiraia na kila mtanzania kwa ujumla kutunza
mazingira na kupanda miti ni hatua moja mbele katika kutunza mazingira
yetu”.Alisema Mh. Suluhu.
Akimkaribisha mgeni rasmi katika
uzinduzi wa kampeni hiyo, mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda
alisema serikali imeweka chuma na minyororo ili kulinda wananchi kuvuka
eneo ambalo si sahihi na kuweza kuhatarisha maisha yao kwa kugongwa na
magari.
Alisema wananchi wanapaswa
kulinda vyuma hivyo kwa kuwa vinasaidia kufanya mazingira yawe mazuri na
kukinga miti na nyasi zilizopandwa kando ya barabara hizo zisiharibiwe.
“Wale wanaopita usiku na wale
wanaoharibu, mtu yeyote akikamatwa ameiba chuma kimoja faini yake ni
kununua vyuma kumi na kuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”.
Tags
SIASA



