Majadiriano Baada ya picha ya pamoja
Na John Banda,Dodoma
WAGANGA Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini wamemlilia Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa kudai tatizo la
ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika baadhi ya vituo vya afya nchini limekuwa likisababisha malalamiko wa
Wananchi.
Akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa
wataalamu wa sekta ya afya kwa niaba ya Waganga hao,Mwenyekiti wa Waganga
hao,Dk Sudi Leonard alisema tatizo la ukosefu wa dawa na vifaa tiba limekuwa
likisababisha malalamiko na manunguniko kwa wananchi.
‘’Mheshimiwa
Makamu wa Rais pamoja na mambo yote lakini tunachangamoto ya ukosefu wa dawa na
vifaa tiba hali hii imekuwa ikisababisha malalamiko kwa Wananchi’’
‘’Mchakato
wa upatikanaji wa dawa pia umekuwa ukichukua mchakato mrefu kutoka MSD mpaka
kufika sehemu husika pia kuna hili kundi la watu maalum na wao wanapokosa
hulalamika’’alisema
Pia alisema
kwa sasa wanaupungufu wa asilimia 49 ya watumishi na madaktari katika sekta ya
afya hali ambayo huwalazimu kufanya kazi katika mazingira magumu.
‘’Tunaiomba
serikali itoe fursa ya ajira kwani kwa sasa kuna Zahanati 334 ambazo
zinasimamiwa na wahudumu ambao sio wataalamu wa afya’’alisema
Kwa upande
wake Samia alisema kutokana na tatizo la
ukosefu wa dawa nchini serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 70 kwa ajili
kumaliza tatizo hilo.
Samia
alisema dawa hizo zitaenda moja kwa moja katika
vituo vya afya vilivyopo hapa Nchini.
‘’Tumetenga
Bilioni 70 kwa ajili ya kumaliza tatizo la dawa nchini pia tumetenga jumla ya
shilingi bilioni 85 kwa ajili ya kupunguza deni MSD nia yetu ni kutaka huduma
za afya ziwe zenye ubora’’alisema
Pia alisema
Serikali inampango wa kujenga Kiwanda cha dawa katika Mkoa ya Simiyu ili kuweza
kukabiliana na tatizo la dawa hapa nchini.
‘’Tuna
maombi ya viwanda kama 8 au 9 vya dawa na sasa tunahangaika kufungua kiwanda
kikubwa cha dawa katika Mkoa wa Simiyu lengo likiwa ni kukabiliana na taizo la
dawa pamoja na ile azma yetu ya Tanzania ya Viwanda
Vilevile
aliitaka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii,jinsia Wazee na Watoto kuhakikisha
utafiti wa taaluma na dawa za asili zinazotumika nchini zinasajiliwa baada ya
mamlaka husika kudhibitisha zinakidhi viwango.
‘’Tiba
mbadala na tiba asili ni taaluma yenye asili ya kiafrika tuliyorithi kutoka kwa
mababu zetu kutoka na uhitaji wake mkubwa
ninaagiza Wizara kuhakikisha waganga wa tiba asili wote wanasajiliwa na
wanafahamika’’alisema
Pia
aliwataka wataalamu hao wa afya kutosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu
wale wote wanaobainika kukiuka maadili na viapo vyao vya kazi.
‘’Niwatake
wote kujitadhmini utendaji kazi wake na kubadilika mkubuke kuwa mustakabali wa
afya za wananchi upo mikononi mwenu’’alisema
mwisho
|