Manchester United wanaikaribisha
Manchester City leo katika mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la Ligi
maarufu kama EFL, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Old Trafford.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na upinzani unaochangizwa na uhasama wa makocha wote wawili kwani kuna kipindi walifikia kutopeana hata mikono wakati wakiwa La Liga Jose Mourinho alikuwa anakinoa kikosi cha Real Madrid na Pep Guardiola akiwa Barcelona timu hizo zimekuwa na upinzani mkubwa hivyo wanakutana tena Uingereza hii ikiwa ni mara ya pili ya kwanza ilikuwa kwenye Liga Mourinho alikubali kichapo cha magoli 2-1 toka kwa Guardiola.
City hawashinda michezo mitano kwenye michuano yote na meneja wao Pep Guardiola ataendelea kufanya mabadiliko ya kikosi chake.
“Baadhi watacheza leo. Nahitaji
kuona wachezaji mazoezini halafu ndiyo natoa maamuzi yupi acheze na yupi
asicheze,” amesema Guardiola
United pia mwezi huu bado
hawaonja ladha ya ushindi kwenye ligi mwezi huu ikiwa ni pamoja na
kupewa kipigo cha aibu cha magoli 4-0 kutoka kwa Chelsea Jumapili,
lakini Guardiola amesema “mara zote amekuwa akiwaheshimu wapinzani wake”
“Ni timu yenye ubora wa hali ya
juu. Tumewazidi alama, ikiwa ni sawa uwiano wa michezo miwili tu,”
amesema Guardiola ambaye kwenye mchezo wa Premier League waliokutana
mwezi September alishinda 2-1.
“Michezo ya mahasimu ina uzito wa kipekee. Tutajaribu kucheza kwa umakini wa hali ya juu ili kupata matokeo.”
Guardiola ameongeza kwa kusema
kuwa angependa kuona mshambuliaji wake raia wa Argentina Sergio Aguero,
ambaye amekuhuwa akihusishwa na kuhama klabuni hapo akibaki kwa muda
mrefu zaidi”.
“Nina furaha sana na Sergio.
Ningependa kumwona anabaki na kuendelea kucheza pamoja nasi. Ni mchezaji
wa aina yake,” Guardiola amesema.
Dondoo za Mechi kwa timu hizo:
Manchester United wameshinda
mechi mbili tu Kombe la ligi kai ya sita zilizopita dhidi ya Manchester
City (sare 1, kufungwa mara 3), japokuwa hawajapoteza mechi tatu
walizokutana Old Trafford.
Mara ya mwisho kwa timu hizi
kukutana kwenye Kombe la Ligi ilikuwa ni msimu wa 2009-10 kwenye nusu
fainali ambapo United walishinda kwa wastani wa magoli 2-3, baada ya
kushinda 3-1 Old Trafford.
Mara zote ambazo Man City
wamewaondosha mahasimu wao mashindanoni kwenye Kombe la Ligi,
wamefanikiwa kubeba kombe hilo (1969-70 na 1975-76).
Kwenye michuano yote, Man City
wameshinda mechi nne kati ya sita zilizopita katika Uwanja wa Old
Trafford (sare 1, kufungwa mara 1).
Ushindi mara mbili kati ya tatu
wa Jose Mourinho dhidi ya Pep Guardiola kama meneja umetokana na mechi
za michuano ya ligi (mara moja kwenye Champions League, na mwingine
kwenye Kombe la Copa Del Rey).
Kwenye michuano yote, Guardiola
ameshindwa kupata matokeo kwenye mechi tatu za ugenini akiwa na Man
City. Amewahi kucheza mechi nne za ugenini bila ushindi katika historia
ya maisha yake ya ukocha (ilikuwa ni mwezi March 2009).
Tags
MICHEZO KIMATAIFA