Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora
akisoma taarifa ya utekelezaji wa Shirika la Posta kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Shirika hilo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Shirika la Posta Dkt. Haruni Kondo akisoma taarifa ya uendeshaji wa
Shirika hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo
uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kwenye begi lilobeba
vitendea kazi vya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta
katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi
hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………..
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi teule ya Shirika la
Posta kutumia fursa zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika
hilo.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo
wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta katika
ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano leo Jijini Dar es
Salaam.
“Nashukuru kwa kuwa mmekubali
uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga
mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafta mapato
na shirika hili la Posta lina vyanzo vingi lakini bado halijatumika
vizuri na hivyo naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele”
Alisema Prof Mbarawa.
Aidha Waziri Mbarawa ameitaka
bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye
kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya
wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata
matokeo mazuri na amesisitiza kuboreshwa kwa mahusiano kati ya
watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.
Waziri Mbarawa ameagiza bodi iyo
teule kusimamia huduma mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa
uadilifu ili vilete tija kama ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo
kuwa serikali imejipanga kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza mzigo
wa utendaji wa shirika hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Msaafu Haruni
Kondo amemhakikishia waziri uyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya
Shirika hilo na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinapatikana kama
alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa maendeleo wa
shirika hilo.
Tags
BIASHARA