
Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limetangaza kuanza rasmi kwa mashindano ya ligi kuu ya wanawake nchini Tanzania ambayo yanatarjiwa kuanza rasmi tar mosi Novemba kwa uzinduzi utakaofanyika mjijini Dodoma siku hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho hilo Karume jijini Dar es salaam leo, Alfred Lucas ambaye ndiye msemaji wa shirikisho, alisema ligi hiyo imepangwa kuanza kama ilivyokusudiwa na kuwa usajili wa wachezaji utabaki kama ulivyo kwakuwa hakukuwa na uthibitisho juu ya madai ya vilabu vilivyokata rufaa juu ya usajili.
“Kama tulivyosema hapo mwanzo kuwa ligi kuu ya mpira wa miguu kwa upande wa akina dada itaanza tar moja Novemba na uzinduzi wake utafanyika mjini Dodoma, kwa tamngazo hili pia wale waliokataa rufaa wajue kuwa rufaa zao zimetupwa kwakuwa hazikuwa na vielelezo muhimu hivyo usajili utabaki kama ulivyo” Alisema Lucas.
Kwa mujibu wa ratiba siku ya ufunguzi inaonyesha kuwa kuwa kutakuwa na mechi kati ya Baobab Queens ya Dodoma watakaoingia dimbani kucheza na Panama Fc kutoka Iringa .
Naye Baruan Muhuza mkurugenzi wa michezo wa kampuni ya utangazaji ya Azam ambao ndiyo wenye haki ya kuonyesha michuano hiyo, alisema kuwa wao wamejipanga kuonyesha michezo mitatu kila siku ya mechi hizo na kwamba wana uhakika wataonyesha bila kuwa na wasiwasi na kwa ufanisi mkubwa kama ilivyo kwe ligi kuu ya Vodacom.
“Tumejipanga kuonyesha mechi tatu kati ya nne zitakazokuwa zinachezwa kwa ubora ule ule na tunafurahi kuwa hii itakuwa ni ligi ya kwanza ya wanawake katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kwakuwa hakuna nchi yenye ligi ya wanawake kama itakavyokuiwa kwetu, nasi tutaonyesha michezo hiyo kama tufanyavyo kwa wanaume” Aliserma Muhuza
Akizitaja sababu za kupeleka ufunguzi wa ligi hiyo mjini Dodoma , Muhuza alisema, wameamua kupeleka huko kama sehemu ya kuunga mkono hatua ya serikali kuhamia Dodoma lakini pia michuano hiyo itachezwa wakati vikao vya bunge vikiwa vinaendelea na hivyo viongozi wengi wa serikali pamoja na wabunge walioko Dodoma watapata fursa ya kushuhudia sherehe hizo za kihistoria za ufunguzi wa michuano hiyo.
Hii itakuwa ni ligi kuu ya kwanza ya wanawake kuchezwa katika ukanda wa CECAFA, huku shikisho la soka hapa nchini likikusudia kuiotumia michuano hiyo kama sehemu ya kuimarisha vikosi vya timu za taifa za wanawake hapa nchini.
Tags
MICHEZO KITAIFA