Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo (pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel
Chongolo(kwanza kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido
Mhe. Esupat Mulupa wakielekea kukagua ujenzi wa mabweni katika Shule ya
Sekondari Longido .
Afisa Elimu wa Halmashauri ya
Longido Ndg. Gerson Mtera(mbele) akisoma taarifa ya ujenzi wa mabweni ya
Shule ya Sekondari ya Longido wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wilayani
hapo.
Ujenzi unaendelea katika mabweni ya Shule ya Sekondari Longido na hivi ndivyo yanavyoonekana kwa sasa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akishirki kwenye ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Longido.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo(aliyesimama) akizungumza na walimu pamoja na watumishi
wasio walimu katika Shule ya Sekondari Longido wakati wa ziara ya Kikazi
Wilayani hapo.
Baadhi ya walimu na watumishi wa Shule ya Sekondari Longido wakiwa kwenye Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (hayupo pichani)
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe.
Daniel Chongolo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo wakati wa kikao na walimu wa Shule ya Sec. Longido.
…………………………………………………………………..
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo amechangia mabati 136, mifuko ya Saruji 30 pamoja
na Fedha taslimu Tsh 500,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa
mabweni mawili yaliyoungua moto hivi karibuni katika Shule ya Sekondari
Longido.
Rc Gambo ametoa msaada huo wakati
wa ziara yake ya Kikazi wilayani hapo ambapo alitembelea Shule hiyo na
kukuta wanafunzi wakilala madarasani tangu Mabweni hayo yalipoungua na
uongozi wa Shule hiyo kuamua kutumia madarasa hayo katika kipindi hiki
cha mpito wakati wakiwa wanaendela na ujenzi wa mabweni hayo ambayo
ujenzi wake unagharimu zaidi ya Tsh Mil 45.
Akisaoma taarifa ya ujenzi wa
mabweni hayo Afisa Elimu Sekondari Bw.Gerson Mtera alisema endapo
wangetumia Mkandarasi ujenzi huo ungegharimu zaidi ya Ths Mil 75 lakin
kwa kuwa wanajenga kwa kutumia mafunzi wa jamii pamoja na wataalamu wa
Halmashauri mabweni hayo yatagharimu Tsh Mil 45 tu.
Nimeona jitihada za uongozi wa
Wilaya pamoja Shule katika kukabiliana na changamoto hii na jitihada
zenu hakika sio za kupuuzia na mimi kama Kiongozi wa Mkoa nawiwa
kuchangia kazi hii ili iweze kukamilika haraka na wanafunzi warudi
katika malazi yaliyo bora na madarasa hayo yaweze kutumika kwa shughuli
stahiki alisema Gambo.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa
alikutana na walimu pamoja na wafanyakazi wasio Walimu kusikiliza
malalamiko na kubaini baadhi wa walimu kutolipwa malimbikizo ya Fedha za
Likizo pamoja na watumishi kuajiwa kwa zaidi ya miaka kumi pasipo kuwa
na mkataba wala barua ya ajira kutoka kwa Mwajiri wake.
Akiongea katika Kikao hicho Mhe.
Gambo alisemani ni muhimu kwa kila Halmashauri kuwajali watumishi wake
haswa walimu na wafanyakazi wa kada za chini ili kuwaongezea ari ya
kufanya kazi na kuwatia moyo waweze kutumikia Taifa hili kwa uzalendo
sio kila siku mnatoa vipaumbele kwa watumishi wa Kada za juu kufanya
hivi mnasababisha matabaka yasiyo ya lazima katika utendaji kazi wenu wa
kila siku.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe.
Daniel Chongolo aliahidi mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwa atasimamia ipasavyo
wote wanaohusika na ujenzi wa mabweni ya Sekondari ya Longido ili
kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa na kumhakikishia kwamba
mpaka mitihani ya Kidato cha nne itkapoanza wanafunzi hao watakua
wameshahamia kwenye Mabweni hayo na madarasa hayo yatatumika kwa ajili
ya kazi hiyo na baadae wanafunzi wataendelea kuyatumia katika masomo
yao.
Pia aliongeza kuwa atafuatilia
malimbikizo ya Fedha za waalimu wanazodai kwa ajili ya Likizo ili
kuangalia uwezekano wa kuwalipa kutoka katika Mapato ya Halmashauri na
kuwaagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kushushulikia malalamiko ya
watumishi wote ambao hawana barua za ajira hadi sasa.
Kuanzai wiki ijayo Mkurugenzi
pamoja na Menejiment ya Wilaya kupitia vikao vyenu mliangalia suala hili
kwa makini na Bodi ya Ajira iweze kuketi ili watumishi hawa waweze
kupata haki yao.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo yuko katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi katika
Wilaya ya za Mkoa wa Arusha amabapo mpaka sasa amekwisha tembelea Wilaya
ya Ngorongoro.
Tags
ELIMU