BANDA MEDIA BLOG

WIZARA IMARISHENI HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA-MAJALIWA

ddm1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya mkoa wa Dodoma Oktoba  1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ddm2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo ya kuboresha usafi wa mazingira ya hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati alipoitembelea  hospitali hiyo Oktoba 1, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ddm3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa maelekezo ya kuboresha usafi wa mazingira ya hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakati alipoitembelea  hospitali hiyo Oktoba 1, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ddm4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma baada ya kutembelea hospitali hiyo Oktoba 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ddm5
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao baada ya kuitembelea hospitali hiyo, Oktoba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ddm6 ddm7
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Bi. Fatuma Yassin wa Swaswa Dodoma wakati alipotebelea hospitali ya mkoa wa Dodoma Oktoba 1, 2016.  Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ddm8
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Bi. Magreth Kapinga  wa Mpwapwa wakati alipotembelea  hospitali ya mkoa wa Dodoma Oktoba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuboresha upatikanaji wa huduma katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa kuhakikisha inakuwa na  dawa na vifaa tiba vya kutosha.
Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Oktoba Mosi, 2016) wakati alipotembelea hospitali hiyo akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.                               
Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikishirikiana na uongozi wa mkoa huo katika kumaliza changamoto zinazoikabili hospitali hiyo manispaa nazo zinajukumu la kuboresha utoaji wa huduma za afya katika zahanati na vituo vya afya.
“Waziri Afya atawajibika kuimarisha hospitali ya mkoa na Manispaa  waimarishe huduma katika zahanati zote na vituo vya afya ndani ya mkoa kwa kuziwezesha kuwa na majengo ya kutosha, kuongeza idadi ya watumishi na kuhakikisha zinakuwa na dawa na vifaa tiba,” alisema.
Aidha, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na isitokee watu wakakosa dawa au vipimo kwa sababu mmoja wao amechukua na kupeleka kwenye duka lake binafsi.
Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. James Kiologwe kutafuta vijana watakaoweza kusafisha na kutengeneza bustani ya maua kwenye eneo lililoko karibu na uzio wa hospitali hiyo ili liwe na mandhari ya kuvutia.
Awali Mganga Mkuu wa mkoa, Dk. James Kiologwe aliiomba Serikali kupandisha hadhi hospitali hiyo na kuwa ya kanda kwa sababu mbali ya mkoa wa Dodoma, hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wengine kutoka mikoa ya Iringa, Tabora, Singida na Manyara.
Akizungumzia upatikanaji wa tiba wakati Serikali imeanza kuhamia Dodoma, Dk. Kiologwe alisema mkoa huo unaweza kukabiliana na ongezeko la watumishi kwa una hospitali tano ambazo zina madaktari bingwa wa fani mbalimbali.
“Tunazo hospitali tano ambazo ni Benjamin Mkapa, Mirembe, DCMC, St. Gemma na hii ya ya Rufaa ya Mkoa zenye uwezo wa kutoa huduma za upasuaji, huduma kwa mama na mtoto, magonjwa ya moyo, mishipa, figo na saratani na huduma za mionzi,” alisema.
Katika hatua nyingine Dk. Kiologwe alisema hospitali hiyo imedumia wagonjwa wa nje 158,375 walipatiwa huduma katika hospitali hiyo katika kipindi cha Julai 2015 hadi Juni 2016 ambapo ni sawa na wastani wa wagonjwa 13,198 kwa mwezi.
“Magonjwa yanayoongoza kwa wagonjwa wa nje ni mivunjiko, shinikizo la damu, kisukari, homa ya mapafu na upungufu wa damu,” alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG