picha ya pamoja na mgeni Rasmi
Na John Banda, Dodoma
WAANDISHI wa habari mkoani Dodoma wamesema kutokana na
kutopata ushirikiano katika kitengo cha Habari na mawasiliano cha ofisi ya mkuu
wa mkoa huo kinawanyima wakazi wake na watanzania kwa ujumla haki ya kupata
habari ambayo ni haki yao kikatiba.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Clabu ya Waandishi wa
habari mkoani Dodoma [CPC] Wakati wa mkutano wake mkuu wa mwaka uliofanyika
juzi katika ukumbu wa New Dodoma Hotel ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mndeme kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Jordan Rugimbana
Mwenyekiti huyo alisema hakuna ushirikiano kwa muda mrefu
sana kati ya waandishi wa habari wa mkoa huo na kitengo cha habari cha ofisi ya
mkuu wa mkoa na hata wanapojaribu kuyatengeneza wao wanagonga ukuta
Alisema pamoja na jitihada walizowahi kufanya hazikufanikiwa
kwa mhusika/ wahusika wa kitengo hicho mara zote wapo bize na mambo yao huku
wakisahau kuwa habari ni haki ya wanadodoma na watanzania kwa ujumla
“nitakuwa sijawatendea haki kama sitaanza na changamoto
inayotutesa muda wote kuhusu maswala ya kihabari na kitengo cha Habari na
Mawasiliano cha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Kutokana na hali hiyo tuliamua mimi na kamati yangu kuwaita maafsa wa habari na mawasiliano wa
taasisi zote kubwa za kiserikali na za binafsi ambapo tuliomba ukumbi na
tukapewa kwa maandishi katika ofisi za mkuu wa mkoa cha kushangaza ni kuwa
hakukuwa na mwakakilishi yoyote toka ofisi hiyo, hivyo tunakuomba mkuu wa
wilaya utufikishie ujumbe wetu kwa mkuu huyo ili azifanyie kazi”, alisema
Aidha alisema kuhusu ubaguzi wa vyombo vya habari kwa kutaka
kufanya kazi na vyombo ambavyo yeye anaita vikubwa vya Luninga na baadhi ya
Magazeti bila kutaka kufanya kazi na redio za kijamii zilizopo mjini Dodoma
wakati hivyo ndivyo vinasikika vijijini na maeneo yasiyo na umeme bila tatizo
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya Chirstina Mndeme aliwataka
waandishi hao kutokatishwa tama na baadhi ya watu hasa linapokuja swala la
kutaka kuwahabarisha watanzania huku akiwataka wanadodoma kuwa wazalendo kwa
kuanza na kupenda vya kwao ikiwemo kuzigeuza changamoto kuwa fursa
|