BANDA MEDIA BLOG

Tukio hili lilistahili kuwa ‘tuta’?

fume
Lilikuwa ni tukio ambalo liliacha maswali mengi kwa wadau wa soka kwa ni penati au haikuwa penati? Hiyo ilikuwa ni katika mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Old Trafford.

Ulikuwa ni mchezo wa nguvu huku ufundi ukiwa ni kwa asilimia chache, nafasi pia zilikuwa chache kutokana na kila timu kuwa makini kuhakikisha hairuhusu goli.
United waipata nafasi nzuri ya kupachika bao la kuongoza kipindi cha kwanza lakini mlinzi wao wa kulia Antonio Valencia  alionekana kuangushwa kwenye box na beki wa The Gunners Nacho Monreal lakini mwamuzi hakutoa penati.
Je Manchester United walitakiwa kuzawadiwa penati kwa tukio hilo?
Kwa upande wa Mourinho bila shaka ilikuwa ni tuta, alionekana kukasirishwa na mwamuzi baada ya kutoamuru kupigwa penati na akaonekana akilalama kwa fourth official.
Siku za hivi karibuni, Mourinho aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo dhidi ya Bournemouth kutokana na vitendo vyake vya kuwalalamikia waamuzi.
Vitendo vya Mourinho kupishana na waamuzi imekuwa ni kawaida kwenye maisha yake kwa sababu mara zote anadhani waamuzi wanainyima timu yake penati kwa makusudi.
Mara kadhaa Manchester United ilifaidika na mikwaju ya penati kwenye uwanja wa Old Trafford wakati wa utawala wa Fergie huenda labda Mourinho anataka timu yake iendelee kunufaika kama nyakati za Fergie.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG