BANDA MEDIA BLOG

Nyambui amwaga jezi SHIWATA


mpi
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa Riadha, Suleiman Nyambui ametoa jezi seti sita kwa timu zilizoshiriki mashindano ya soka ya maveterani yaliyofanyika jana uwanja wa Shule ya msingi, Kitunda.
Nyambui aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali hizo zilizoshirikisha timu sita mmoja ilitokea Kisarawe kocha huyo ambaye kwa sasa anafundisha riadha nchi ya Kifalme ya Brunei aliwaasa wachezaji wasikate tamaa kutokana na umri kuwa mkubwa bali wafanye mazoezi mara kwa mara.

Alisema watanzania tunashindwa kufikia malengo kama zamani alivyowahi kufikia kutwaa ushindi ya kukimbia katika mashindano ya Olyimpiki 1980 n.a. Gilbert Bayi kutokana na kulewa sifa na kuendeleza anasa kwa kulewa pombe.
Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na SHIWATA,timu ya Kitunda Veteran iliibuka mabingwa baada ya kuichapa Vituka mabao 4-2 katika fainali iliyokuwa na ushindani ikichochewa na wachezaji waliowahi kuwika Simba.
Victor Costa Nyumba ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo akichezea Kitunda Veterani pamoja na Emmanuel Gabriel huku Vituka ikimchezesha Japhet Mamboleo ambaye naye aliwahi kuchezwa Simba.
Kitunda Veterani ilizawadiwa kikombe sh.150,000, vyeti cha ushiriki na uwanja wa kujenga,Vituka ilipata sh.150,000 na vyeti cha ushiriki,Kivule Veteran ilishika nafasi ya tatu na kuzawadiwa sh.100,000 na Stakishari Veterani ilikuwa timu yenye nidhamu na kuzawadiwa sh. 50,000.
Timu ya Mwanga All Stars ya Keko Mwanga na Kisarawe Veterani Ilipata vyeti cha ushiriki
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema mashindano hayo yalitanguliwa na mengine ya sarakasi, mpira wa kikapu na Mchezo as kujilinda Wu-Shu

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG