Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe
ametembelea shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga (Green
House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam
wake leo Ijumaa.
Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao
walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao
wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu Byakanwa
kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la
Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe.
Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo lenye ukubwa wa
hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba
hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.
Tags
SIASA
