Mohamed Maulid mkazi wa Pugu Kinyamwezi ambaye ni mfanyakazi wa Tanesco
na mtoto wake Sumaiya Mohamed (3), wamemwagiwa mafuta ya moto na mke
wake (Severine) baada ya mke huyo kupewa talaka siku mbili kabla ya
tukio hilo.
Maulid alisema baada ya kumpa mwanamke huyo talaka alikuwa anampiga tu
tarehe kuwa ‘ntaondoka kesho, ntaondoka kesho.’ “Na nilivyokuwa naenda
kazini nilimuuliza utaondoka saa ngapi akasema ataondoka jioni, nikahisi
kwamba anaona aibu kuondoka mchana ataondoka jioni,” amesimulia.
“Nilikuwa nimelala nikasikia kama moto umelipuka, nilikuwa nimelala
fofoFo, nikashtuka nikaanza kupiga kelele nimemwagiwa maji ya moto
nikapiga kelele majirani wengine wakanisikia wakatoka nje, wakaenda
kumuangalia na mtoto wakakuta na mtoto naye kaungua sana na yupo kule
wodi ya watoto.”
Baadaye majirani wakanisaidia wakamuita dereva taksi nikawaambia
nikimbizeni hospitali kwa uzima wangu. Mimi nilipomwagiwa mafuta yale,
nilikurupuka nikakuta mlango upo wazi na wakati mlango nilikuwa
nimefunga nimefunga na misumari kwasababu nilikuwa simuamini tena
kwanini hataki kuondoka, nikakuta mlango ule umefunguliwa na wa nyuma
umefunguliwa na mtoto wangu alimwagiwa mafuta kichwani nilimuona.”
Jirani yao aliyejulikana kwa jina la Sofia Ngumbali alisema, “usiku
mwanamke huyo alienda jikoni kuchemsha mafuta na akapanga viti akarukia
chumba cha mumewe kufika pale mlangoni kwa kuwa funguo alikuwa
hajaichomoa akafungua mlango na akachukua mafuta akaja kuwamwagia yeye
na mwanae waliokuwa wamelala pamoja.”
“Yule mwanaume alivyokurupuka akapiga kelele majirani tulijua mwizi
kukurupuka tukamkuta anagalagala nje anasema kuwa mkewe amemmwagia
mafuta, na sisi tulikuwa tunaona wanaishi kwa amani wakitoka wanatoka
wote na kurudi wote kwahiyo ya ndani mtu huwezi kujua yaliyopo ndani ya
ndoa,” aliongeza jirani huyo.
Kwa upande wake mama wa mtuhumiwa huyo akiwa na mjukuu wake katika
hospitali hiyo aligoma kutoa ushirikiano alipokuwa akihojiwa na
waandishi.
Tags
MAHUSIANO
