NAIBU
Waziri Tamisemi ,Selemani Jafo amemtaka afisa Uvuvi wa halmashauri ya
wilaya ya Mafia,mkoani Pwani kuhakikisha anadhibiti uvuvi haramu wa
kutumia mabomu na kama uvuvi huo utaendelezwa afisa huyo atawajibishwa.
Sambamba na hayo ameeleza halmashauri ya wilaya ya Mafia hali
sio shwari hivyo watendaji wajitume kwa kufuata kasi ya serikali iliyopo
madarakani.
Alisema,
matumizi ya mabomu yamekua mwiba kwa mazalia ya samaki baharini ambayo
madhara yake ni makubwa kwa nyakati zijazo ambayo yanatakiwa kudhibitiwa
mapema.
“Nikisikia uvuvi haramu wa kutumia mabomu unaendelea huku
samaki wakifa na kupunguza ongezeko, afisa uvuvi kazi hana, kwasababu
tunaendelea kutoa maagizo lakini hakuna usimamizi mzuri”alisema Jafo.
Alisema, uvuvi haramu matumizi ya mlipuko na nyavu hazistahili kutumika katika kuvua samaki na ni jambo la hatari.
Aliwataka watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani baadhi ya mambo yanaendelea kuzorota kwa kutokua na mabadiliko.
Jafo alisema, athari kubwa itakua kwa kwa watu ambao watashindwa kufuata maelekezo ya viongozi.
Aidha alisema Halmashauri ya wilaya ya Mafia bado hali si
nzuri kutokana na utendaji mbovu na kama wapo watendaji wataendelea
kutowajibika na kubadilika hatua zitachukulia.
Tags
HABARI KITAIFA