Zaidi ya watu 900,000 wamesaini petition ya kutaka kusitishwa kwa ziara
ya Donald Trump nchini Uingereza kufuatia uamuzi wake wa kupiga marufuku
waislamu kuingia Marekani
Mipango ya Trump kuzulu nchini Uingereza, ilitangazwa saa 48 zilizopita
baada ya waziri mkuu, Theresa May kueleza kuwa Rais huyo ameukubali
mwaliko toka kwa malkia.
Petition hiyo inadai kuwa Trump hapaswi kualikwa nchini humo kuepuka
kumdhalilisha malkia. Uamuzi wa Trump kuzuia raia wa nchi 7 za Kiislamu
kuingia nchini Marekani umepingwa vikali.
Tags
KIMATAIFA

