Nahodha wa timu a taifa ya Tanzania , Mbwana Samatta
amezidi kuwasha
moto katika ligi kuu ya Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro League baada
ya kuifungia timu yake ya KRC Genk bao moja katika ushindi wa mabao 3-0
walioupata wakiwa ugenini usiku wa Ijumaa hii dhidi ya Sint-Truiden.