Mkuu wa Mkoa Dar es salaam kupitia Account yake ya Instagram Ameandika
Ujumbe unaotafsiriwa ni kama kuwajibu wakosowaji wote ambao wanabeza na
kudharua kile anachokifanya.
Katika Ukarasa wake wa Instagram Paul Makonda Ameanza kwa kuandika
"Usiogope Mbwa Mwitu, unapoanza kuchipuka katika wazo lako…. na ndio
maana kuna wimbo wa mwimbaji anaitwa Ephraim kutoka Zambia naupenda
sana“
Pia akaenda mbali zaidi na Kusema kuwa Mungu hajalala kama watu
wanavodhani hii ikiwa na Maana kuwa kila akifanyacho yu Pamoja na Mungu
na Mungu anamsimamlia kwa kile anachokifanya
“Wimbo unasema wewe ni Mungu usielala…………. Mungu wetu hajalala, mantiki
ya Mungu kutokulala hachoki na kuna mahala nimekupa katika hii mistari
anasema utataka jambo nawe litakua, imani utakayokua nayo itakusukuma
kutaka jambo litakua“
“Mbwa Mwitu ni wale watu ambao wanabweka tu… unaanza jambo wanakubwekea kiasi kwamba wanakufanya mpaka unakata tamaa”
Tags
BIASHARA HARAMU
