Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Vijana kutoka Asasi mbalimbali za
kijamii nchini wameshauri Wakuu wa Mikoa yote hapa nchini kutekeleza
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli la kupambana na watumiaji na wasambazaji wa dawa za kulevya.
Vijana hao wametoa kauli hiyo leo
jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya
kuunga mkono juhudi zinafanywa na uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Wamesema mapambano dhidi ya dawa
za kulevya siyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam pekee Paul Makonda,
yapaswa yafanywe na viongozi wote wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa
Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wananchi wenye kupenda maendeleo mema ya nchi
hiyo.
Wametoa wito kwa wananchi
kusaidia katika utoaji wa taarifa za watu wanaojihusisha na biashara
hiyo haramu ya dawa za kulevya katika Ofisi zao za Mitaa.
Wameongeza kuwa Tanzania ya
Viwanda haiwezi kufanikiwa ikiwa nguvu kazi inaharibika kutokana na
matumizi ya dawa za kulevya na kuwageuza vijana ambao ndio tegemeo kuwa
tegemezi.
Aidha vijana hao wameonya baadhi
ya Viongozi na Wanasiasa kuacha tabia za kuwakatisha tamaa viongozi
waliojitoa kupambana na biashara hiyo haramu kama vile Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda.
Wasema kuwa kufanya hivyo
kunawatia mashaka na kuwahisi kuwa wao na ni wahusika katika biashara
hiyo haramu ambayo inaliteketeza Taifa.
Vijana hao wametoa siku tatu kwa wafanyabiashara wakubwa kujisalimisha wenyewe la sivyo watawataja.
Vijana waliounga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wanatok
Tags
BIASHARA HARAMU

