*Ataka waandike barua ya kuomba radhi kwa Rais Magufuli
*Aagiza Waziri wa Biashara aje na timu yake
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akionyesha Mifuko ya mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara ikiwa
na maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo inazalishwa nchini Kenya.
Mifuko hiyo ambayo ilishuhudiwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa Februari
19, 2017 wakati alipotembelea kiwanda hicho, ilimkera sana na aliuagiza
uongozi wa kiwanda hicho kumuandikia barua Rais John Pombe Magufuli
ya kumuomba radhi kwa kitendo hicho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akionyesha Mifuko ya mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Kagera ikiwa
na maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo inazalishwa nchini Kenya.
Mifuko hiyo ambayo ilishuhudiwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa Februari
19, 2017 wakati alipotembelea kiwanda hicho, ilimkera sana na aliuagiza
uongozi wa kiwanda hicho kumuandikia barua Rais John Pombe Magufuli
ya kumuomba radhi kwa kitendo hicho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza kabala ya kutembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani
Manyara kuanza awamu ya pili ya ziara yake mkoani humo Februari 19,
2017. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba
na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa ManyaraDkt. Joel Bendera. Kushoto ni
Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi.
Baadhi ya wananchi na viongozi wa
Mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza kabla ya kutembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani
Manyara, Februari 19, 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Raymound
Mushi akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa kwenye kiwanda cha mbolea cha Minjingu ambako Mheshimiwa
Majaliwa alianzia awamu ya pili ya ziara ya mkoa wa Manyara, Februari
19, 2017.
Waziri wa Kilimo , Mifugo na
Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipotembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara,
Februari 19, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mgodi wa kiwanda cha mbolea cha Minjingu wakati alipotembelea
kiwanda hicho mkoani Manyara, Februari 19, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara, Februari 19, 2017
Baadhi ya wananchi na viongozi wa
Mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza kabla ya kutembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani
Manyara, Februari 19, 2017.
Mifuko ya mbolea ya kiwanda cha
Minjingu mkoani Kagera ikiwa na maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea
hiyo inazalishwa nchini Kenya. Mifuko hiyo ambayo ilishuhudiwa na Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa Februari 19, 2017 wakati alipotembelea kiwanda
hicho, ilimkera sana na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kumuandikia
barua Rais John Pombe Magufuli ya kumuomba radhi kwa kitendo hicho.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza
mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya
Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.
Kutokana na hilo, Waziri Mkuu
amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais
Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari
22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.
Ametoa agizo hilo leo (Jumapili,
Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya
Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri
Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba
za kitaifa.
“Nilikuja kukagua kiwanda baada ya
kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti
wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati
niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani
ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.
“Ni kwa nini mifuko hii ina anuani
ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali
kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani?
Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe
radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda
ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”
Akiwa ndani ya kiwanda hicho,
Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County
Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani
ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha
Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro
Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini
mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.
Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.
Pia amesema atamwagiza Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na
wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara
(FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.
“Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.
“Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class
duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la
kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii
kweli?”
“Nataka wakati namaliza ziara
nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa
kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.
Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo,
Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu
kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu
ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.
Waziri Mkuu kesho anaendelea na
ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom,
kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari
Singland.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.
Tags
BIASHARA