Meli mbili za Mv. Ruvuma na Mv
Njembe zikiwa katika cherezo katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela
Mkoani Mbeya, zikiwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kufanyiwa
majaribio ndani ya Ziwa Nyasa Mwishoni mwa Februari, 2017.
Bw. Juma Nassoro akipaka rangi
meli ya mizigo ya Mv Ruvuma, ikiwa ni hatua za mwisho wa ukamilishaji wa
uundaji wa meli hiyo yenye uwezo wakubeba tani 1000 za mizigo
itakayokuwa ikifanya safari zake Ziwa Nyasa, wakti Ujumbe wa Serikali
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda Biashara na
Uwekezaji na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ulipofanya ziara katika
Bandari ya Itungi, wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Kiongozi wa Ujumbe wa Serikali
unaotembelea kujionea shughuli za biashara mipakani mkoani Mbeya, Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban
(Katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof.
Adolf Mkenda (kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya (kushoto), wakisikiliza maelezo ya Kaimu
Mkuu wa Bandari ya Itungi iliyoko Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, Bw.
Ajuaye Msese (hayupo pichani) wakati viongozi hao walipotembelea bandari
hiyo kujionea ujenzi wa Meli mbili za mizigo unaoendelea chini ya
Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA.
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Itungi,
Wilayani Kyela mkoani Mbeya, Bw. Ajuaye Msese akitoa maelezo mafupi
kuhusu Bandari ya Itungi, na majukumu yake kwa ujumla kwa wageni
waliotembelea Bandari hiyo mkoani Mbeya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd, inayounda meli
tatu katika Bandari hiyo, Bw. Saleh Songoro, akielezea historia fupi ya
kampuni yake iliyoingia mkataba na Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA
kuunda meli tatu Ziwa Nyasa, baada ya Ujumbe wa Serikali ukiongozwa na
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban,
ulipotembelea Bandari hiyo wilayani Kyela mkoani Mbeya
Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro
Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha mchoro wa meli mbili
za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja anazoziunda kwa
ajili ya matumizi katika Ziwa Nyasa, katika Bandari ya Itungi, Wilayani
Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutembelewa na ujumbe wa Serikali
unaofuatilia masuala ya biashara mipakani mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro
Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha moja kati ya ya meli
mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja anazoziunda
kwa ajili ya matumizi katika Ziwa Nyasa, katika Bandari ya Itungi,
Wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutembelewa na ujumbe wa Serikali
unaofuatilia masuala ya biashara mipakani mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionyesha mchoro wa
meli mbili za mizigo za MV Ruvuma na Mv Njombe alizoziunda wakati Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wa
kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Balozi Hassan
Simba Yahya (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara
na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa tatu kushoto) walipozulu Bandari ya
Itungi, iliyoko Wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro
Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akiongoza ujumbe wa Serikali
kutoka Wizara za Fedha, Uwekezaji, na mambo ya Ndani kujionea kazi ya
ujenzi wa Meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 za
mizigo kila moja zinazojengwa katika Bandari ya Itungi iliyoko Wilayani
Kyela mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro
Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha mfumo wa kuongoza
meli katika chumba cha nahodha wa meli ya Mv Njombe, huku Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda, Biasha na Uwekezaji Prof Adolf. Mkenda, akiangalia
kwa makini mfumo huo wa kisasa namna unavyofanya kazi.
Baadhi ya wajumbe wa Serikali
waliofanya ziara katika Bandari ya Itungi mkoani Mbeya kujionea uundwaji
wa meli mbili za mizigo wakishuka kwenye ngazi baada ya kumaliza
kukagua meli ya Mv Njombe inayotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine
Transport Ltd inayoshughulika na kutengeneza vyombo vya usafiri vya
majini katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Benny Mwaipaja, WFM, Kyela
UJENZI
wa meli mbili za mizigo katika Bandari ya Itungi wilayani Kyela Mkoani
Mbeya, MV Njombe na MV Ruvuma, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98 na
kwamba meli hizo zinatarajiwa kufanyiwa majaribio Ziwa Nyasa, mwishoni
mwa mwezi Februari na kukabidhiwa rasmi Serikalini mwezi Machi, 2017
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Songoro MarineTransport Ltd ya Jijini Mwanza,
inayounda meli hizo, Mhandisi Saleh Songoro, amesema hayo wakati ujumbe
wa Serikali ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Fedha na
Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea Bandari hiyo ukiwa
katika zaira ya kukagua hali ya biashara mipakani mkoani Mbeya.
Amesema
kuwa kukamilika kwa meli hizo mbili za mizigo za kisasa zenye uwezo wa
kubeba tani elfu moja (1,000) za mizigo kila moja na kugharimu shilingi
bilioni 11, kutaiwezesha Kampuni hiyo kuanza kuunda meli nyingine ya
tatu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo.
Pause: Mhandisi Saleh Songoro- Kampuni ya Songoro MarineTransport Ltd
Pamoja
na meli hizo, Mhandisi Songoro amesema kuwa mradi huo pia umewezesha
kujengwa kwa cherezo cha kwanza na cha pekee kitakacho iwezesha Mamlaka
ya Bandari Tanzania-TPA katika uundaji wa meli na kuzifanyia matengenezo
meli nyingine za ndani na nje ya nchi zikiwemo Malawi na Msumbiji.
Kaimu
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bandari ya Itungi, Bw.
Ajuaye Msese, amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuunda meli hizo
ulikuwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa vyombo vya
baharini vya kusafirisha abiria na mizingo ndani na nje ya nchi kupitia
Ziwa Nyasa.
Pause: Bw. Ajuaye Msese-Kaimu Mkuu wa TPA, Bandari ya Itungi
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, , pamoja na kupongeza kazi kubwa iliyofanywa
na mkandarasi mzawa, Songoro Marine Transport Ltd, kuunda meli hizo,
wamesema kuwa kukamilika kwa meli hizo kutachochea biashara na mapato ya
serikali kupitia shughuli za usafiri na usafirishaji katika Ziwa Nyasa.
Pause: 1. Prof. Adolf Mkenda- Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
2. Bi. Amina Khamis Shaaban- Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
Prof.
Mkenda amesisitiza kuwa Serikali itaangalia uwezekano namna ya kumtumia
Mkandarasi huyo, Bw. Saleh Songoro, kuunda meli nyingi zaidi za ndani
na nje ya nchi ili kukamata soko hilo la utengenezaji wa meli kitaifa na
kimataifa hatua itakayoliletea Taifa sifa, kukuza uwekezaji na ajira.
Ujenzi
wa Meli zote tatu, mbili za mizigo pekee, na moja ya mizigo na abiria,
umekadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 20 na utakuwa
umetekeleza ahadi ya Serikali ya muda mrefu ya kuboresha usafiri wa
abiria na mizigo kupitia Ziwa Nyasa, ambapo unatarajiwa kukuza biashara
kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji, kusisimua uchumi wa wakazi wa
wilaya ya Kyela na ukanda wote wa Kusini.
Aidha
kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo kutapunguza matukio ya ajali za mara
kwa mara zinazogharimu maisha ya watu wengi wanaotumia Ziwa Nyasa,
linalo tajwa kuwa la pili kwa kuwa na mawimbi makali na la tano kuwa na
kina kirefu cha maji duniani.
Tags
USAFIRISHAJI