RAIS SAMIA AWAPONGEZA WASICHANA WA SERENGETI GIRLS

Timu ya wasichana ya Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Girls), imefuzu kuingia robo fainali za Kombe la Dunia baada ya kutoka sare ya 1-1 na Canada, katika mchezo wa mwisho wa kundi D kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kwa umri huo.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Rais Samia ameonyesha kufurahishwa na wasichana hao kutokana na mafanikio hayo makubwa waliyayafikia kwenye michuano hiyo.
”Mmenifurahisha sana Watoto wangu @serengetigirls kwa kuandika historia ya kufuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 nchini India. Mmefanya jambo kubwa kwa nchi yetu Tanzania na nawatakia kheri katika hatua ya robo fainali.”- Rais Samia Suluhu Hassan
Wasichana hao Watanzania wanatarajia kumenyana na wenzao kutoka nchini Corombia katika hatua hiyo ya Robo Fainali
Mchezo huo ulipigwa katika dimba la DY Patil Navi – Mumbai nchini India, ambapo wamefikisha jumala ya pointi 4 baada ya sare hiyo.