Afrika Kusini Kubinafsisha Bandari yake Kwa Uphilipino
Afrika Kusini inakusudia kubinafsisha shughuli za bandari katika mpango wa muda mrefu ili kuboresha shughuli na kuongeza ufanisi kutokana na bandari hizo kukosolewa kwa muda mrefu kwa kutofanya kazi vizuri, miundombinu iliyochakaa na msongamano.
Transnet,
kampuni inayomilikiwa na serikali ambayo inahusika na bandari na mfumo
wa usafirishaji, ilitangaza kuichagua kampuni ya Kimataifa ya Huduma za
Makontena ya Kimataifa (ICTSI) kutoka Ufilipino kama mnunuzi
aliyechaguliwa kwa ubinafsishaji wa bandari ya makontena ya Durban
kwenye Gati 2, mchakato ulioanza mwaka 2021.
Baada
ya kufanya mapitio ya kampuni zilizowasilisha maombi, Transnet
iliripoti kuwa imechagua ICTSI na itaunda kampuni mpya ya pamoja kwa
ajili ya uendeshaji wa gati hiyo. Transnet itamiliki zaidi ya asilimia
50 ya kampuni mpya ambayo itakuwa na mkataba wa miaka 25 ambao unaweza
kuongezwa hadi miaka 30 kulingana na wakati wa operesheni ya kuongeza
kina katika Gati ya Kaskazini kwenye Gati 2.
"Ushiriki
wa sekta binafsi kwenye Gati 2 ni muhimu sana katika kubadilisha upya
Bandari ya Durban kuwa bandari kuu ya makontena. Ushirikiano katika Gati
2 ni hatua kubwa kwenye programu yetu ya kuwaleta wataalamu wa
kimataifa kuboresha ufanisi katika bandari zetu, na inakuza vizuri
mipango yetu ya kuhamasisha sekta binafsi katika maeneo yaliyotambuliwa
kwa ukuaji," amesema Portia Derby, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Transnet.
Wakati wa kutangaza makubaliano hayo,
walibainisha kuwa si tu itaboresha upangaji wa vifaa katika bandari za
Afrika Kusini lakini pia itachangia sana katika kuchochea biashara ya
kuuza nje na kuagiza. Durban imekuwa ikipoteza shehena katika miaka ya
hivi karibuni kutokana na changamoto zake za uendeshaji.
