Lissu Atakiwa Kuripoti Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashtaka Kufuatia Kauli Zake
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu
amedai kuitwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam
kesho tarehe 20 Julai 2023.
Kwa mujibu wa barua
iliyotolewa jana tarehe 18 Julai 2023 kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilimtaka Mwanasheria huyo machachari
kufika katika ofisi hiyo kutokana na kauli alizozitoa tarehe 15 Julai
2023 na kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Tarehe
15 Julai 2023, Lissu anadaiwa kutumia maneno yasiyo na staha kumjibu
Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu uwekezaji wa Kampuni ya DP World katika
bandari ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa barua hiyo ya wito, Lissu anatakiwa kufika kwa mahojiano ili kukamilisha uchunguzi wa maneno hayo.
Kupitia
ukurasa rasmi wa akaunti yake ya Twitter, Lissu ameandika hivi; “Baada
ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu.
DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi
nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo
kuwakabili.
-------------------
