KIWANDA CHA MKULAZI CHAANZA KUZALISHA SUKARI
Kukamilika kwa kiwanda cha kuzalisha sukari Mkulazi kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kumetajwa kuwa kutawezesha kutoa ajira za moja kwa moja na za muda mfupi kwa vijana zaidi ya 5000.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini mfuko wa hifadhi wa jamii (NSSF) Mwamini Juma Malemi alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua kiwanda hicho ambacho hadi sasa kimekamilika kwa asilimia 100 na tayari kimeanza kazi ya uzalishaji wa sukari.
Aidha alisema kuwa sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho itaanza kupatikana madukani hivi karibuni na pia kutakuwa na duka maalumu litakalouza sukari kwa bei elekezi ya kiwanda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Mkulazi Dkt. Heridelita Msita alisema kuwa kiwanda hicho kimeanza kazi na amewahakikishia watanzania upatikanaji wa sukari ya kutosha kutoka kwenye kiwanda hicho.

