BANDA MEDIA BLOG

KUDHURUMIWA MALI KWA WAJANE BAADA YA KUFIWA NA WAUME ZAO KWASABABISHA SIMANZI...


Mwenyekiti wa Jukwa la Uwezeshaji Kiuchumi Mkoa wa Dodoma, Mary Mabara, akielekeza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wanawake wa jana wa kata ya Nkuhungu, Jijini humo..

    Mlezi wa Kundi la wanawake wajane la kata ya Nkuhungu, Ashura kimwaga                                            akiongea jambo katika mkutano huo.

                                     NA JOHN BANDA, DODOMA

                                        BANDA MEDIA ONE.COM

KINA Mama wajane Zaidi ya 280, wa Kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma wamesema Changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo ni kudhurumiwa na kunyapaliwa na Ndugu wa  walikuowa Wenza Wao hali ambayo imekuwa ikiwakwamisha kiuchumi na kujikuta wakishindwa kulea watoto na Familia walizoachiwa.

Hayo yamebainishwa na Mlezi wa Umoja wa Wajane hao, Ashura Kimwaga wakati alipokuwa akisoma Risala kwenye mkutano wa kundi hilo uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mtube iliyopo kata ya Nkhungu Jijini Dodoma, leo Disemba 29,2023 ambapo amesema hali hiyo inawasababishia simanzi kubwa.

 “ndugu Mgeni Rasmi kutokana na wengi wetu kudhurumiwa mali zilizoachwa na marehemu, kutengwa na kunyapaliwa kumetusababishia kushindwa kabisa kujimudu kiuchumi, tukishindwa kulea familia na hata kuwasomesha watoto”, amesema

 Mgeni Rasmi katika Mkutano huo wa Wajane Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi wanawake Mkoa wa Dodoma, Mary Mabaya amewataka kuunda vikundi vya ujasiliamali na kuandika shughuli ambazo wanaweza kuzifanya.

 “nimeambiwa mpo wajane kutoka mitaa saba ya kata hii mkiwa 284, hivyo niwaombe undeni vikundi vya ujasiliamali na mimi kwa sababu nina ujuzi kufundisha utengenezaji wa Bidhaa mbalimbali, nitawafundisha na kuwafungulia akaunti katika moja na mabenki yetu hapa Dodoma, kisha tutawaomba wawape na mikopo yenye riba nafuu”,

Aidha amesema inabidi kila Mjane awe na imani kwa Mwenyezi Mungu, wajiamini wasikae kwa kubweteka badala yake inapotokea Fursa yoyot ya kiuchumi basi, waichangamkie kwa kujiamini.

 Awali Mwenyekiti Taasisi ya CALVINE WALINGOZI FAUNDATION, Caroline Sanga, aliwataka wajane hao kuondokana na Unyonge wa kufiwa na waume zao badala yake wanatakiwa kuona huo ndiyo mwanzo wa maisha mapya na ya kujisimamia wenye. 

Diwani wa Viti Maalum Jiji la Dodoma, Rosemary Nitwa akisistiza jambo wakati alipokuwa akitoa salamu kwa wajane hao.
Mwenyekiti Taasisi ya EALVINE WALINGOZI FAUNDATION, Caroline Sanga, Akiongea jambo
Mjumbe wa kamati kuu ya Idara ya Fedha Uchumi na Mipango wa Jukwaa la wanawake Dodoma, Ester Kimwel akuongea jambo katika mkutano huo
Katibu wa UWT Tawi la Samamba Nkuhungu,  Wema Sehaba akielezea jambo mbele ya Mkutanao huo
                                                     Picha ya pamoja baada Mkutano huo


Mchungaji Nickson Botesigirwe akichangia jambo katika mkutano huo wa wanawake wajane
Mchungaji Elizabert Mwakalasya wa Kanisa la PCGT Nkuhungu akifafanua jambo mkutanoni hapo 
Maombi na Salama yaliyofanywa na Mgeni Rasmi, Mary Mabaya Kama kiapo cha Kujikomboa kiuchumi kwa wanawake hao Wajane,







Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG