BANDA MEDIA BLOG

No title

 VIONGOZI WA UAK WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI NA WELEDI KATIKA MADARAKA YAO


                         

                            NA  JOHN BANDA,

                         BANDA MEDIA ONE.COM

                       ...................................................

VIONGOZI wa taasisi ya Umoja wa Amani Kwanza (UAK), ndani na nje ya Tamnzania, wametakiwa Kuyatumia Vizuri Madaraka waliyopewa kwa kuteuliwa huku wakitakiwa kuzinagatia Weredi bila kubaguana.

 Pia Wanataasisi hiyo ambao walikuwa wamerudia nyuma kiutendaji, kutohudhuria vikao, mikutano na matukio yote ya Taasisi hiyo kutokana na sababu mbalimbali wanatakiwa kurudi na kushirikiana na wenzao kwa mazingira yatakuwa bora zaidi.

Hayo yamesemwa leo Disemba 30,2023 na Makamu Wa Rais wa Taasisi ya Umoja wa Amani kwanza, alex Mnyangabe wakati wa ziara ya Viongozi wa Kitaifa wa taasisi hiyo walipoutembelea mkoa wa Dar es laam

Mnyangabe amesema kuwa taasisi hiyo inatakiwa kupewa nguvu ili iwe Kubwa kuliko mtu mmoja mmoja ambao ndio walikuwa chanzo cha kuwakatisha tamaa Wengine kutokana na kuyatumia vibaya madaraka waliyopewa

“hii ni taasisi lazima iwe kubwa kuliko mtu mmoja mmoja, viongozi wa ngazi zote wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weredi na nidhamu kwa wanaowaongoza,

Tumefungua pia mlango wa kupokea maoni na ushauri, siyo majungu kutoka kwa watu wa chini ambao siyo viongozi kwa lengo la kuendelea kuboresha”, amesema

Amesema kuwa hivi sasa kunaonekana kuna mmeguko kati ya wanataasisi wa zamani na  wapya ambapo wengine ni kama wanatengwa hawapewi nafasi wala thamani yao, “hilo hatutalikubali na tumeanza kulifanyia kazi na leo mhe. Rais Dr. Willison Munguza amemteua Mitete kuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweka uwiano”, amesema

Aidha amesema taasisi hiyo inakwenda kuanzisha Mfumo wa Tehama kwa lengo la kuwaingiza wanataasisi wote katika mfumo, na kwamba Akaunti ya Taasisi itaunganishwa ili kila mtu atakafanya malipo yoyote atambulike na viongozi wote wa taifa.

“kutakuwa na uwazi kwenye fedha, miradi yote ya taasisi ikiwemo ya Kutengeneza vitamburisho, Sare za wanataasisi na mingine itakayojitokeza hapo baadae kutakuwa na kampuni maalum ndani ya taasisi itakayosimamia hilo

Jambo jingine Makamu huyo amesema Taasisi hiyo inafanya kazi ya kumsaidia Rais wa Nchi na serikali yake kazi huku kwenye jamii kwa kujitolea, hivyo kila mtu awe na moyo wa kutoa nguvu zake kwa uzalendo wa nchi yake zaidi kuliko kutarajia kupata kitu…

Ziara hiyo inatarajia kuifikia Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibr kwa lengo la kuiimarisha taasisi hiyo. 


Rais wa Taasisi ya Umoja wa Amani kwanza Dr. Willison Munguza akionyesha moja ya vyeti vya pongezi ambavyao Taasisi hiyo imekuwa ikipata, kutoakana na mchango wake katika jamii, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Tasisi hiyo Netto Ndirito
Rais wa Taasisi ya Umoja wa Amani Kwanza, Dr. Willison Munguza wa katikati, Makamu wa Rais Alex Mnyangabe na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Netto Ndirito wakionyeshana Cheti cha pongezi kilichotolewa na Serikali ya Uganda hivi.

                                                                      Mkutano ukiendelea


                                     Picha ya Pamoja baada ya Mkutano huo kuahilishwa

               

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG