BANDA MEDIA BLOG

HII HAPA SIMULIZI YA MWALIMU ''SINGLE MOTHER'' ALIYEKIMBIA KAZI KISA NGONO

 

                          Mwalimu Doris Peter akiwa kwenye majukumu yake

UALIMU ni wito, pia ni kazi kama zilivyo kazi nyingine za kitaaluma si kazi za watu waliopotea au kufeli Maisha usione mwalimu anaongea kwa sauti ya juu, kwa vitendo vya mikono na hata mwili mzima wakati mwingine akiimba na kucheza Pamoja na wanafunzi wake ukamchukulia poa.

Mnachotakiwa kujua ninyi madaktari, Wahandisi, Tehama, Waongozaji wa Ndege, Meli na wa huko jeshini, Waandishi wa Habari, Wanasayansi na wengine ambao sijawataja hapa. Wote tulipita mikononi mwa walimu bila kujali hali na mapito yao ya kimaisha yalikuaje.

Hapa BANDA MEDIA tumekutana na Mwalimu Doris Peter anayefundisha Shule ya Msingi Yusufu R. Makamba iliyopo Wilayani Temeke jijini DSM, aliyepata nafasi ya kutusimulia hadithi yake ya alipotoka mpaka kufikia Kuwa kiongozi wa Fikra katika Ualimu.

Mwalimu huyo anasema baada ya kumaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Vituka mwaka 2007, alianza kazi ya kuuza Duka la Baba mmoja aliyekuwa Jirani yao ambapo hata hivyo mnamo Mwaka 2008 alilazimika kuiacha kazi hiyo akidai kukimbia uzalilishwaji kingono uliokuwa ukimnyemelea kutoka kwa Bosi wake huyo.

“nililazimika kuacha kazi hiyo kutokana na kukumbana na uzalilishashwaji wa kingono tena kutoka kwa bosi wangu mwenye umri mkubwa kama Baba yangu,

baada ya kumkatalia aliamua kuanza kuninyanyasa na kuninyima mshahara wangu. Niliamua kuondoka badala ya kupoteza heshima yangu. Nilijisikia kupungukiwa, lakini kwa hakika nilikuwa najinusuru”, anasema kwa hisia

Aidha DORIS aliamua kujiunga na Dada yake aliyekuwa fundi wa kushona nyumbani kwao, akajifunza kushona chini yake baada ya kujua naye akawa anawafundisha wenzake tena kwa upendo mkubwa, kitendo kilichomfanya Dada yake huyo anayeulikana kwajini la Jane, kung’amua kipaji cha Ualimu ndani yake, akaamua kumshauri akasome Ualimu.

“sikuwahi kusoma chuo cha ushonaji bali nilijifunza chini ya dada Jane pale nyumbani, na ndiye aliyenishauri kusomea ualimu baada kuona ninavyowaelekeza wanzangu kushona kwa umakini mkubwa na kwa upendo”, amesema

Mnamo mwaka 2009 alijiunga na chuo cha ualimu Mpwapwa na kuhutimu ngazi ya cheti mwaka 2011, ambapo mwaka uolifuata wa 2012 alipata ajira ya kwanza katika shule ya msingi Saku mbagala alipofanya kazi mpaka 2017 na baadae kuhamishiwa shule ya msingi kiwanja cha ndege hadi 2025 alipohamishiwa Yusufu R. Makamba huko Temeke, ambako yupo hadi sasa akiwa mwalimu wa kawada.

Mwalimu Doris anasema mpaka leo anashindwa kusahau pigo la kumpoteza kaka yake wa Pekee Mwaka 2016, hali iliyosababisha huzuni kubwa na mzigo wa Maisha  na hali ya upweke kuongezeka kutokana  na wao kuzaliwa watu tu kwa wazazi wao.

Anaongeza kuwa akiwa kazini , aliamua kujiendeleza kielimu ambapo  Mwaka 2021 hadi 2023 alisoma uongozi katika Chuo cha ADEM, kwa ajili ya kujengea uwezo wa Uongozi wa elimu. Badala ya kuwa mwalimu wa Darasani tu bali kuwa kiongozi wa Fikra katika Elimu na kujinyakulia cheti cha Diploma

Mwalimu Doris anatanabaisha kuwa, Ndoto yake kubwa ni kusoma hadi kufikia ngazi ya Daktari (PhD) au Profesa katika masuala ya Elimu.

“natamani kusoma kwa kengo la kuja kuchangia kwenye sera, mitaala na mifumo ya elimu inayotambua kwamba wanafunzi hawaji darasani wakiwa tupu wanakuja na historia, maumivu, malezi, umasikini, upweke na ndoto”, anasema na kuongeza

anasema changamoto za kiuchumi zinamsababisha kuiona safari hiyo ionekane ngumu, lakini anaamini ndoto inayozaliwa kwenye maumivu huwa na nguvu ya kipekee, hivyo ataendelea kusonga nayo mpaka atoboe.

Mwalimu huyo ambaye Pamoja na Ualimu, pia ni mama wa Watoto watatu, anayejua uchungu wa kulea, peke yake ( Single Mother), anajua maumivu kejeli za walimwengu, shinikizo la kimapenzi, mzigo wa kiuchumi, na uchovu wa kuwa mama na baba kwa wakati mmoja. Lakini pia anajua nguvu ya mwanamke asiyekataa haanguki.

Anasema kitu cha ziada kwake ni kuwa mwalimu anayewaelewa Watoto kwa kina hasa wanaopitia maumivu ya kimya kimya kwa kuwaangalia na hivyo kuchukua hatua ya kuwasaidia kisaikolojia.

Anaweka wazi ndoto yake kuwa bado anaota kuona Elimu inayojenga fikra, maadili na nidhamu. atamani kuwa mwalimu atakayegusa jamii, na kuanzisha au kufanya kazi na taasisi itakayosaidia Single Mothers na watoto wanaolelewa na mzazi mmoja, ili kizazi kijacho kipate msaada na mwanga zaidi.

Hata hivyo Pamoja na yote hayo anapenda kujiendeleza kwa kusoma makala, vitabu ikiwemo kufuatilia majarida mbalimbali  Pamoja na kuandika makala mbalimbali ambazo zinaweza kuleta matokeo chanya katika jamii na kuwavusha wengine mahala wanapopita ama kuwasaidia kwa namna moja au nyingine, ikiwemo kuwafariji.

Kwa waliokata tamaa mwalimu Doris anatumia misemo hii kusema, Kuanguka si mwisho bali ni daraja.

Kama yeye aliyelelewa bila baba, akapoteza kaka, akapitia unyanyasaji wa kingono, akakosa matokeo, akalea watoto peke yake bila mwenza na bado akasimama, wewe pia unaweza kusimama tena amua kuamka leo uanze moja na mia inakuta

            Doris ni ushahidi kwamba:

Hata ukianza gizani, unaweza kuwa taa kwa wengine.

Hata ukiumia, unaweza kuwa uponyaji wa wengine.

Na hata ukiwa peke yako, bado unaweza kujenga kizazi.

Safari bado inaendelea kubwa ni kuondoa uoga na kuianza.

MWISHO

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG