BANDA MEDIA BLOG

No title

 MHE. BALOZI BYAKANWA ATEMBELEA MABANDA YA WAJASIRIAMALI KUTOKA TANZANIA

Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa akiangalia bidhaa za wajasiriamali wa Tanzania alipowatembelea katika Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura, Burundi. 


Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa akizungumza na watendaji kutoka Tanzania alipowasili katika Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura, Burundi.

Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ally Msaki akimweleza jambo Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa wakati alipotembelea wajasiriamali katika Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course), Bujumbura, Burundi. 

           


.................................................................

Na; Mwandishi Wetu – Bujumbura, BURUNDI

 

BALOZI wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa ametembelea mabanda ya Wajasiriamali wanaoshiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayoendelea kufanyika Bujumbura, Burundi.

 

Akiwa katika maonesho hayo, Balozi Byakanwa amewataka wajasiriamali kuendelea kufanya biashara zao kwa tija na ufanisi, pia amewahimiza kutumia fursa hiyo kutafuta masoko zaidi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

 

Vili vile, ameipongeza Serikali kwa kuwezesha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania kushiriki maonesho ambayo yanasaidia kukuza ajira na kupanua masoko ya bidhaa na huduma zao.

 

MWISHO

 


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG