BANDA MEDIA BLOG

No title

 MWENYEKITI WA BODI YA EWURA AKAGUA MIUNDOMBINU YA MAMLAKA YA MAJI TUKUYU

Mhandisi Barnabas Konga ( kushoto) kutoka Mamlaka ya Maji Mbeya, akimweleza Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof Mark Mwandosya( aliyeketi kulia) kuhusu maendeleo ya mradi wa maji Mbaka, wakati kiongozi huyo alipotembelea chanzo cha maji cha Mto Mbaka, 18 Desemba 2023. Mamlaka ya Maji Mbeya, ndiye msimamizi wa mradi huo.

Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Mark Mwandosya ( mwenye mkongojo) katika picha ya pamoja na watendaji wa EWURA, Mamlaka ya Maji Tukuyu na Mamlaka ya Maji Mbeya, katika chanzo cha maji Mbaka, wakati wa ziara ya kikazi ya kufuatilia na kutathmini utendaji wa Mamlaka ya Maji Tukuyu na maendeleo ya mradi wa maji Mbaka.

.............

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, Prof Mark Mwandosya, amefanya ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji wa Tukuyu ( Tukuyu WSSA), Jumatatu, 18 Desemba 2023 kwa lengo la kukagua miundombinu ya maji na kufuatilia utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji Mbaka, wenye thamani ya bilioni 4.5 uliopo Kitongoji cha Mbaka juu, Kijiji cha Isebe, Kata ya Itagata, Tukuyu, Rungwe.

Mradi huo, unatajiwa kuimarisha huduma ya maji kwa asilimia 95 na kuongeza upatikanaji wa maji katika mji wa Tukuyu, ambapo kwa sasa huduma inapatikana kwa saa 13 tu kwa siku.

EWURA husimamia utendaji wa mamlaka za maji nchini ili kuhakikisha huduma zake zinakidhi ubora, kanuni za afya, utunzaji wa mazingira na zinapatikana kwa uhakika na kwa gharama nafuu.




Chanzo cha Maji cha Mto Mbaka, nje ya kidogo ya mji wa Tukuyu, katika kitongoji cha Mbaka Juu, kijiji cha Ibese, kata ya Itagata, kitakachohudumia mradi wa maji Mbaka.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG