BANDA MEDIA BLOG

No title

 

TUKIMBILIE TOBA



Adeladius Makwega-MWANZA

“Sauti ya Mtu Aliyae Nyikani, itengenezeni Njia ya Bwana na Yanyosheni Mapito Yake.”

Hayo ni maneno ya utangulizi ya mahuburi ya Padri Samson Masanja katika misa ya kwanza ya Dominika ya 2 ya Majilio ya Mwaka B wa Liturujia ya Kanisa , Disemba 10, 2023 katika Kanisa la Bikira Maria-Malkia wa Wamisionari, Parokia ya Malya, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.

Padri Masanja aliongeza kuwa ujio ya Yesu Kristo ni kuyahukumu mataifa yote kwa haki,

“Nawaombeni tuendelee kutafakari neno la Mwenyezi Mungu linatotukumbusha juu ya ujio wa Masiha, sisi tunaosikia ujumbe huu tunapewa kazi ya kujitayarisha ambapo mahali palipopinda , palipokwaruza ambapo hapajanyoka kuwekwe sawa ili kupitika, hilo ndilo jukumu linatolewa katika dominika ya leo.”

Padri Masanja alisema kuwa atakapokuja Masiha atawatenganisha wanadamu katika makundi mawili, wale wenye haki kwenda kupata uzima wa milele na wasio haki kwenda katika moto wa milele.

Padri Masanya aliwaomba waamini kukimbilia toba.

Misa hiyo pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,

“Uamshe viongozi na watawala wa dunia, washirikiane na Kanisa katika kuleta haki na amani duniani, Ee Bwana Twakuomba Utusikie.”

Hadi misa hiyo ya kwanza inamalizika majira ya saa moja ya asubuhi, hali ya hewa ya Malya na Viunga Vyake bado ni jua na mvua, huku mahindi mashambani wengine yakiliwa kwa kuchemswa na kuchomwa na wengine wakiendelea kupanda, nao wakulima wa mpunga baadhi yao wakitayarisha majaruba , huku vitalu vya mpunga tayari vimeshaotesha mipunga hiyo na imechipua. Huku umeme ulikatika majira ya saa 2 ya asubuhi na kurejea saa 12. 00 jioni.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG