BANDA MEDIA BLOG

No title


WAFANYABIASHARA SABASABA JIJINI DODOMA WAHOFIA AFYA ZAO KUTOKANA NA UCHAFU .....!!!!!!

 Wafanyabiashara wa bidhaa za sokoni wakisubiri wateja, katika soko la sabasaba jijini Dodoma, Huku maji machafu yanazalishwa na taka zilizopo kwenye Dampo la dharula lilijianzisha baada ya kutoondolewa kwa taka hizo kwa kipindi kirefu.. 



                
..............................................................

NA JOHN BANDA, DODOMA
 WAFANYABIASHARA Ndogondogo wa Bidha za Sokoni  wanaofanyia Biashara zao ndani ya iliyokuwa Stendi ya Daladala ya Sabasaba, wamelalamikia kukidhiri Kwa uchafu uliozagaa na kutengeneza Dampo katika soko Hilo Hali ambayo inatishia afya zao iwapo kutatokea Magonjwa ya Mlipuko....

Wakiongea na waandishi wa habari baadhi ya Wafanyabiadhara hao wamesema kitendo cha Taka hizo zilizochanganyika na Aina mbalimbali za Matunda yakiwemo maembe ni hatari kwa afya zao, kwani taka hizo zinakaa kwa muda mrefu kiasi cha kuzalisha Funza bila kuchukuliwa na wahusika.

Loyda Rubeni ambaye ni mfanyabiashara sokoni hapo amesema taka hizo zimekuwa zikizagaa katikati ya wafanyabiashara wa matunda, Mbogamboga na bidhaa nyingine za vyakula kwa zaidi ya wiki moja, ambapo kwa sasa  msimu wa mvua unapoanza jijini Dodoma tayari wana hofu ya kupata magonjwa ya mlipuko yanayotokana na Uchafu.

kwa upande wake Paulina Elieza amesema wamekuwa wakifikisha kero hizo kwa viongozi wa jiji lakini majibu ambayo wamekuwa wakiyapata ni ya kukatisha tamaa.

"ukiwauliza wanakwambia mara hawana mafuta au gari limehalibika sasa sisi tufanyaje", amesema na kuhoji

Aidha, wafanyabiashara hao wameiomba serikali kuwaondolea Kero hiyo Kwa kuongeza vifaa vya kuhifadhia na kusombea takataka ili soko Hilo liwe safi

Afisa Afya Mazingira anaeshuhulikia Uthibiti wa Taka Ngumu, Melania Mtui amesema wakati mwingine wamekumbana na changamoto za namna hiyo lakini wanajitahidi, kushughulikia kwa kukodi magari na wakati mwingine kutumia makampuni binafsi na vikundi vya mazingira vilivyopo kwenye kata...

"pamoja na hapo nyuma kuwa na chanagamoto za namna hiyo lakini kuelekea Mvua hizi zilizoanza kunyesha tumejipanga vizuri ili kukabiliana na hali hiyo, 

ni kweli wakati mwingine tumekumbana na Changamoto kama za kuhalibika Kwa magari au mfumo wa kuchikulia mafuta kuchelewa kusoma, hali inayosababisha ucheleweshaji wa huduma hiyo, lakini hata hivyo tunajitahidi kulifanyia kazi swala hilo na hata hivi hi leo tumeshatuma gari kwenda kuziondoa taka hizo katika soko la sabasaba", amesema.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG