UMOJA WA KINA MAMA WAJANE KATA YA NKUHUNGU JIJINI DODOMA, WAANZISHWA WENYEWE WALIA KUKIMBIA NYUMBA ZAO KUTOKANA NA MIKOPO YA KAUSHA DAMU, DIWANI AWAPA FUNGU ATAKA LIWANUFAISHE WOTE
Watalaam Mbalimbali
Mlezi wa Wajane hao Ashura Kimwaga akiselebuka paomoja na kina mama hao
Afisa maendeleo ya jamii Kata za Nkuhungu na Chamwino Sophia Primo akizungumza jambo kwenye Utambulisho huo
Afisa Ushirikishwaji Jamii wa Kata ya Nkuhungu Inspt wa Jeshi la Polisi Amina Hamis Shabani, Akisisitiza jambo wakati alipokuwa akitoa Elimu ya Ukatili wa kijinsia kwenye utamburisho huo
Diwani wa Kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma Daud Mkande akielekeza jambo katika mkutano huo wa utamburisho wa Umoja wa Wajane zaidi ya 200 ulioanzishwa katika kata yake.
.................................................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
KINA Mama wajane wa Kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma wamesema miongoni mwao wamekuwa wanakumbana na Changamoto ya Kukikmbia Nyumba na familia zao Kutokana na Mikopo inayoumiza Maarufu Kama KAUSHA DAMU..
Pia imebainika kuwa akina Mama hao huumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo hali mbaya ya kiuchumi ambayo hupelekea kushindwa kumudu gharama za maisha na kushindwa kumudu Maisha na kuwasomesha watoto wao.
Akisoma Risala Mlezi wa Umoja wa Wanawake hao wajane, Ashura Kimwaga amesema Hali hiyo imekuwa ikiwaumiza akina Mama hao wajane hapa nchini mara wanapoondokewa na wapendwa wao na kujikuta wakijiingiza katika Mikopo Hiyo inayoumiza maarufu kama KAUSHA DAMU.
Vilio hivyo vimesikika leo Novemba 29, 2023 Jijini Dodoma wakati kina mama hao wakikitambulisha kikundi Chao cha Wajane Chenye wanachama zaidi ya 200, katika Kata ya Nkuhungu Kwa serikali ya Kata hiyo ambapo wameomba Kusapotiwa ilikunzisha Mfuko utakaowasaidia kuinuana kiuchumi ..
Aidha kwenye Mkutano huo wa Utamburisho Wataalam mbalimbali wa Serikali katika vitengo vya ustawi wa jamii, Sheria, na Jeshi la Polisi walipokualikwa ili kusikiliza changanoto za akina Mama hao wajane ili kuzipatia ufumbuzi ..
Akiongea Mkutanoni hapo Afisa Ushirikishwaji Jamii wa Kata ya Nkuhungu Inspt wa Jeshi la Polisi Amina Hamis Shabani, Amewataka kina mama hao kupaza sauti hasa wanapokumbwa na vitendo vya ukatili toka Kwa ndugu wa karibu na wapendwa wao waliotangulia mbele za haki..
"Wakati mwingine wanawake wajane wamekuwa wakikimbwa na madhala ya ukatili wa kijinsia toka Kwa ndugu wa waliokuwa watu wao wakaribu baada Tu ya kufariki, niwaombe mpaze sauti ili serikali iwasaidie kutokana na Sheria za nchi", amesema
Kwa upande wake Afisa Usitawi wa Jamii anayeshuhulikia Kata za Nkuhungu na Chamwino Sophia Primo amesema kwenye jamii kumekuwa na changamoto nyingi za ukatili wa kijinsia ikiwemo Kwa wababa ambapo wamekuwa wakishindwa kutoa taarifa kutokana na kujisikia aibu
" Niwaombe kina Baba acheni kufa na Tai shingoni, toeni taarifa ili matatizo yenu ya kunyanyaswa na wake zenu kijinsia yaweze kutatuliwa ..!!
Akimalizia Diwani wa kata hiyo Daudi Mkande aliwapa fungu la kuanzisha mfuko wao na kuwataka liwanufaishe wotebadala ya baadhi ya watu